Makala : Usiyoyajua Kuhusu Mashoto ( Matumizi ya mkono wa Kushoto ) - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Jun 2016

Makala : Usiyoyajua Kuhusu Mashoto ( Matumizi ya mkono wa Kushoto )



KUHUSU MASHOTO
Kwa miaka mingi, jamii nyingi zimekuwa na mila potofu kuhusiana na mashoto. Wengi wamekuwa wakiita mkono wa kushoto kama mkono wa shetani. Jamii nyingi zimekuwa na kawaida ya kulazimisha kuwabadili watoto wao mkono wa kutumia pindi wagunduapo watoto hao ni mashoto. Jamii hizo zimekuwa zikiamini kuwa mashoto ni ulemavu ama mkosi. 

Kwanza Kabisa nianze na kutoa ufafanuzi wa maneno haya kwa Kiswahili yaani mkono wa kushoto na mkono wa KULIA ni utohozi tu kutoka kwa lugha na tamaduni nyingine na utakuta kimantiki hayashabihiani kabisa linapokuja suala la tasfiri kwenda kwenye lugha yetu maarufu ya kiingereza ambayo ni ya pili kwa matumizi nchini.

Nashawishika Kuamini kwamba huenda matumizi ya neno mkono wa kulia unatokana na urithi wa utamaduni wa kutumia mkono huo kwa KULIA CHAKULA na ndio maana wengi wameathirika kisaikolojia tu kwa kuona mtoto anatumia mkono wa kushoto kwa KULA ilihali mkono huo una maarufu wake hasa kwenye maeneo Fulani NYETI ya haja kubwa na ndogo wengi huuita mkono wa kushoto kama ‘kono la mavi’.  Katika Kilatini, mkono wa kushoto umekuwa ukitwa ‘sinitra’ ambayo humaanisha kitu kiovu. 

Kwa Bahati mbaya sana katika makuzi ya hasa kiafrika, utamaduni wa kutumia mkono wa kushoto haujazoeleka sana na ikitokea mtoto amezaliwa mashoto itafanyika kila jitihada kumbadilisha azoee kutumia mkono wa KULIA jambo ambalo si tu kwamba ni ukatili bali pia linadhoofisha na kudumaza maendeleo ya mtoto ……Nikikuuliza swali wewe unayetumia mkono wa kulia itumike nguvu ya kukubadilisha utumie mkono wa kushoto unadhani ni rahisi?

Naamini kabisa kwamba wengi miongoni mwetu tumepitia kadhia hii aidha kwa kutenda ama kutendewa ama vyote

Nikupe habari njema kifupi tu kwamba kama umezaa mashoto basi una miongoni mwa watu wenye Intelligent Quotient (IQ) kali sana duniani

Mpe nafasi ya kuwa independent wakati unamkuza, mwache achague mwenyewe lolote lile, halafu we ndio umrekebishe kama kachagua baya na uwe tayari kumpa maelezo maana wanadadisi kweli... baaada ya kupita kipindi cha utoto (After his/her early teens) utagundua nilichokuambia kuwa ni genious.

Ukweli ni kwamba ubongo wa binadamu umegawanyika katika maeneo makuu (hemispheres) mawili, KUSHOTO NA KULIA, watu wanaotumia upande wa KULIA udhibiti na uendeshaji wa mambo yao mengi (Emotional, Psychological and Physiological control) huwa yanatoka upande wa kushoto, kadhalika watu wanaotumia upande wa KUSHOTO

Si aghalabu sana kukuta Mashoto duniani (yasemekana ni 10% tu) na kwa nchi nyingine kama Urusi ni watu wanaoheshimika sana, mashoto ambao huitwa ‘Levsha’ huhesabiwa kuwa ni mafundi stadi zaidi wa kazi za mikono. Huko Peru, Amerika ya Kusini, kwenye jamii ya Inca, mashoto wanaaminiwa kuwa na uwezo mkubwa sana kiroho na uponyaji. Mtawala wa tatu wa jamii hiyo aliyekuwa mashoto alipewa jina la Lloque Yupanqui likiwa na maana ‘Mashoto aliyebarikiwa’. 

Wengi wao hutokana na urithi ama vinsaba tu mwilini mwao (inheritance/genetically) kama lilivyo suala la mapacha. Inaelezwa kuwa wazazi wote wawili wakiwa mashoto, upo uwezekano wa asilimia 50 kuzaa mashoto, wakati wazazi wote wawili kama si mashoto, wana uwezekano wa asilimia 2 kuzaa mashoto. 

cha kushangaza ni kwamba wazazi wengi huwa wanadhoofisha ama kuduma  watoto wao wanapojua ni mashoto na ni kutokana na kusongwa na mawzo mgando tu (stereotype) na HII SI HAKI KABISA na ina hatari ya kuja kumsababishia matatizo mengi sana ikiwemo tatizo la kumbukumbu na ugumu wa vitu kama mahesabu. Kitaalamu inaitwa Brain Orientation.

...So cha kufanya ni kumuacha na kumtafutia vifaa ambavyo vina encourage left handedness mfano mlango wa chumba chake uwekwe tofauti na mingine, na baadhi ya vifaa kama mikasi iliyotengenezwa maalum kwa left hand people...watu wengi wa namna hiyo huwa wana uwezo mkubwa ,sana katika sayansi, mahesabu kama hawatakuwa discouraged na pia wana uwezo mkubwa sana kimichezo na hasa kama ni wasichana wanakuwa na uwzo wa juu sana wa akili na kujifunza

NIKUPE VIONJO KADHAA KUHUSU MASHOTO
1.    Mashoto wana uwezo mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu kiasi kwamba wengi wao hawatumii shajara (diary) na hawapendi kutumia notebooks wanapomsikiliza mtu akitoa mhadhara. Utagundua kuwa katika maisha yako ya shule wengi wa MASHOTO ambao ni vipanga si wasomaji wa kukomaa sana/kukesha nk.

2.    Mashoto wengi duniani wana miandiko (handwriting) mizuri na yenye kuvutia mno. Na wanao uwezo mkubwa wa kuandika maandishi (herufi na tarakimu) kwa kinyume (toka kulia kwenda kushoto) 

3.    Mashoto wana vipaji vingi zaidi. Mashoto mmoja anaweza kuwa mchoraji, mshairi, mcheza mpira, mchonga vinyago, mwandishi wa hadithi, mbunifu wa mitindo, mbunifu wa bustani, mcheza filamu, mpigapicha, mpambaji, mwanamuziki na vingine vingi. Tizama mfano wa wanasoka wengi mahiri duniani waliopita waliopo na wajao ni MASHOTO na hii pia inagusa kwa michezo mingine kama Tenis na Ndondi (boxing)

4.    Kwa mujibu wa utafiti wa Dr. Alan Searleman wa Chuo Kikuu cha Mt. Lawrence huko New York, Marekani, mashoto wana uwezo mkubwa zaidi wa utatuzi (problem-solving skills).  na kwamba asilimia kubwa ya watu wenye IQ kubwa ni MASHOTO. Katika wabunifu watano wa kwanza wa kompyuta za Mcintosh, wanne kati yao walikuwa mashoto. 

5.      Viongozi wengi mashuhuri duniani waliopita waliopo na wajao ni MASHOTO. Katika marais wanne wa hivi karibuni wa Marekani, marais watatu ni mashoto. Tazama, George Bush mkubwa (mashoto), Bill Clinton (mashoto), George Bush mdogo (kulia) na Barack Obama (mashoto). Na, katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 1992, wagombea wote watatu wakubwa walikuwa mashoto. Uchaguzi wa Marekani wa 2008, wagombea wote wawili Obama na McCain walikua ni mashoto. 

6.    kwa ujumla. Mashoto wanaelezwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa utambuzi (perception). Watafiti wanaeleza pia kuwa mashoto wana mhemuko, mchomo wa moyo ama hisia (emotions) kwa kiasi kikubwa zaidi. Hivyo mashoto wanaelezwa ni watu wenye upendo na huruma kwa kiwango cha hali ya juu sana.

7.    Mashoto wana uwezo mkubwa zaidi wa kufanya mambo mengi sana (multi tasking). Utafiti wa Dr. Nick Cherbuin wa Chuo Kikuu cha London unaonesha kuwa mashoto wana uwezo mkubwa zaidi wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na ndiyo sababu ni wazuri zaidi hata kwenye video games. 

8.    Mashoto wanapenda zaidi wanyama. Jambo la kusisimua ni kuwa dubu (bear) wote ni mashoto. Mashoto wa kiume huwapenda sana paka, na jambo la kushangaza zaidi paka wote wa kiume ni mashoto. (Naomba kukiri kuwa hili jambo linanihusu). 

SIKU YA MASHOTO DUNIANI NI AGUSTI 31

GEOFREY CHAMBUA-MTAFITI NA MCHAMBUZI WA MASUALA YA KIJAMII NA UKOMBOZI WA WANAWAKE KIMAPINDUZI​.

Hata mimi (Mmiliki wa blogu hii )  nikiri kuwa ni mwathirika , na nilipigwa sana ili nibadilishe Mkono, mpaka nikaanza kutumia mkono wa kulia. Ila ninamshukuru Mungu Mtoto wangu wa Kwanza (Glory ) anatumia Mashoto, na ana akili za kutosha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad