MAPISHI ,NA CHEF KILE :Magimbi ya kuchemsha , Nyama Choma na mboga za Majani - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 16 July 2014

MAPISHI ,NA CHEF KILE :Magimbi ya kuchemsha , Nyama Choma na mboga za Majani





Leo hapa nataka tuangalie mapishi ya kula magimbi na nyama choma pamoja na mboga za majani. MAGIMBI – Kwa magimbi ni kawaida tu yamenye kisha kata kwa staili upendayo na yachemshe tu kwa chumvi. Naam yakiwa yanachemka basi tufanye mangine.
MAHITAJI YA KUCHOMA NYAMA
  • Nyama robo kilo steki ( lean meat steak) hii ni ile isio na mafuta kabisa
  • Pilipili manga kwa kiasi
  • Chumvi kwa kiasi
  • Butter kijiko kimoja cha mezani
  • Vegetable oil vijiko 2 vya mezani
KUICHOMA
Sasa kuna namna mbili za kuchoma nyama yaweza kuwa kwa oven au kwa jiko la mkaa moja kwa moja, ni sawa kwa namna zote. Mimi nitatumia oven; Cha kufanya kabla hujanza  kuichoma nyama ni washa oven yako ikae ikipata joto. Kisha weka chombo cha flampeni kwa moto ; weka mafuta vijiko viwili na cha butter kimoja moto usiwe mkali sana. Sasa ile nyama yako ipakae chumvi na pilipili manga kisha weka kwenye mafuta upange mmoja baada ya mwingine, kama nilivyoonyesha katika video yangu hapo juu.
Baada ya kuwa umezichoma pande zote kwa mafuta vizuri ndio muda wa kuiweka katika oven yako na kuiacha ikichomeka taratibu. Hivyo toa nyama katika flampeni kisha weka kwenye ile sahani ya oven ifunike nyama kwa foil paper kisha weka kwa oven – foil paper itasaidia nyama kutobabuka  na ivo kuifanya iiive pasipo kuwa kavu.
Sasa nyama ingali ikiwa kwa oven watengeneza souse kidogo kwa ajili ya kula na nyama pia.
MAHITAJI
  • Kwanza ni ile ile mafuta ilobaki kwa flampeni uliochomea nyama
  • Unga wa ngano vijiko viwili vya meza
  • Vitunguu maji na swaumu
  • Pilipili manga na Pilipili Mbuzi
  • Limao moja
  • Giligilani
KUANDAA HII SOUSE
Weka ile flampeni uloitumia kwa ile nyama awali ikiwa na mafuta yake vile vile…. kisha weka ule unga wa ngani na endelea kuikaanga kwa muda kama vile unauchoma unga – hii inasaidia kuua wanga/ starch katika unga. Ikiwa kama yakauka hivi basi ongeza maji moto kiasi ili kuweza kutengeneza uji uji….. Baada ya hapo weka vitunguu maji na swaumu viwe katika hali vya kukatakata ( chopped ) na ongeza zile spices zingine kama , pilipili manga , pilipili mbuzi, chumvi kwa kiasi utakacho pia kamulia na liamao , weka na giligilani kisha wacha ichemke kwa kama dakika 4 au 5. Hapo souse yako itakuwa tayari.
Usisahau kutupia jicho kuangalia ile nyama yako katika oven inaendeleaje – Sijasema utaichoma kwa muda gani kwani inategemea na aina ya nyama – zingine zinaiva mapema na zingine zinachelewa.
magimbi nyama
Pia nadhani kwa sasa yale magimbi yapo tayari waweza kuyatoa na kukausha maji kama bado yapo – Unaweza pia kuyaweka kwa oven ili kukauka zaidi.

KUANDAA MBOGA YA MAJANI
  • Mboga ya Spinach / chinese kama fungu moja au zaidi kwa kadiri unavyohitaji
  • Chopped Vitunguu maji na swaumu kwa kiwango nusu nusu
  • Chumvi
  • Binzari kidogo
  • butter oil kama kijiko kimoja
Weka chombo chako katika jiko na mafuta kiasi kidogo , kisha weka vile vitunguu maji na swaumu – hapa ni kama wavipasha moto tu maana havitakiwi kuungua pia waweza ongeza chumvi kidogo sana kwa sasa na baada ya kuweka zile mboga ukaongeza tena. Basi weka mboga zako na chumvi kidogo tena. Baada ya hapo funika kwa dakika tano na mboga iko tayari kwa kuliwa.
Naam naamini kwa sasa vyote vimekamilika – jiwekee katika sahani yako uzuri kabisa na enjoy chakula chako. Kwa mapishi zaidi bofya hapa Chef Kile

No comments:

Post a Comment