Select Menu

Advertisement


News

Technology

Lifestyles

Business

Sports

News

MusicsBondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akimsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng kutoka nchini China na kupelekea mpambano huo kuisha ndani ya dakika mbili na sekunde kadhaa kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam usiku huu.
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akiendelea kumsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng yaliyompelekea kwenda chini na kuomba kutoendelea na mpambani huo.
Bondia Chengbo Zheng akimuomba msimamizi wake kumtoa 'Groves' baada ya kushindwa kuendelea na mchezo kufuatia makonde mazito na ya haraka haraka aliyoyapata kutoka kwa Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe (78.2KG) akitangazwa mshindi mara baada ya kumpiga kwa 'KnockOut' Bondia Chengbo Zheng (77.9KG) kutoka nchini China katika raundi kwanza kabisa ya mpambano wao usiokuwa wa Ubingwa uliomalizika usiku huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akimpongeza
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe kwa ushindi alioupata wa kumpiga Bondia Chengbo Zheng kutoka nchini China, na kufanya heshima ya mchezo huo kuendelea kubaki nchini.
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akizungumza na vyombo vya habari.,
Katika mambano ya utangulizi, kulikuwa na pambano hili la raundi nane lililokuwa na mvuto wa aina yake lililowakutanisha mabondia Said Mbelwa (nyeupe) na Shaban Kaoneka. hili lilikuwa na pambano la rusha nirushe, ambapo Bondia Said Mbelwa alifanikiwa kushinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi dakika ya saba ya mpambano huo.
Chukua hiyooooo...

Bondia Paul Kamata (nyeupe) akimsukumia makonde mithili ya mvua Bondia Buta Obed katika mpambano wao usio na ubingwa wa raundi nani, ulichezwa usiku wa leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam. Bondia Paul Kamata alishinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika raundi ya tano ya mchezo hio.


- - - -

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika na Waislamu wengine wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa ziara ya kibinafsi.
Mfalme wa Morocco, Mohammed VI(kulia) akisalimiana na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga mara baada ya kuswalisha Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa ziara ya kibinafsi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akipokea mmoja wa Miongoni mwa Misahafu elfu kumi iliyotolewa na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya kibinafsi na ujumbe wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani Mjimkongwe wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakitoka nje ya Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya Ijumaa leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake kwa ziara ya kibinafsi.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali walihudhuria katika swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja leo,ambapo Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,na ujumbe wake waliswali kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakiwa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja leo,ambapo Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,na ujumbe wake waliswali kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
- - - -


Wachezaji wa Azam Fc wakimpongeza Nahodha wao John Bocco dakika ya 86 baada ya kuwapachikia bao la ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Vodacom VPL leo kwenye Uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini. Bao hilo limeiwezesha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam kuibuka na pointi  tatu muhimu  baada ya kuinyuka Kagera Sugar mabao 3-2 katika mchezo ulifanyika leo Mkoani Kagera.


Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Azam FC, ulioifanya Timu hiyo ya Jijini Dar es Salaam kupanda juu  nafasi mbili kwenye msimamo baada ya kufikisha jumla ya pointi 19 katika mechi 12 za Ligi ilizocheza. 
Mshambuliaji Themi Felix, alianza kuishtukiza Azam FC kwa kuifungia bao la uongozi Kagera Sugar dakika ya 32 kabla ya Mudathir Yahya kusawazisha kwa bao zuri la shuti akimalizia pasi ya kichwa aliyodondoshewa na Bocco kufuatia faulo iliyochongwa na Erasto Nyoni.


Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilitoka uwanjani zikiwa nguvu sawa. Kipindi cha pili Azam FC ilikianza kwa kasi kubwa ikitaka kupata bao la uongozi lakini mabeki wa Kagera Sugar walikuwa kizuizi kikubwa kwa washambuliaji wa mabingwa hao wakiokoa hatari zote. 
Mwamuzi wa mchezo wa leo, Mathew Akrama kutoka Mwanza, aliamuru penalti ipigwe langoni mwa Azam FC baada ya beki Aggrey Morris kumfanyia madhambi Ally Nasoro ndani ya eneo la hatari, na penalti hiyo ilifungwa na Felix. 
Baada ya bao hilo, mabadiliko ya wachezaji watatu yaliyofanywa na Kocha Mkuu wa Azam FC kwa nyakati tofauti ya kuwatoa Gonazo Ya Thomas, Gadiel Michael na Jean Mugiraneza na kuingia Shaaban Idd, Frank Domayo na Khamis Mcha, yaliongeza uhai kwa timu hiyo na kupelekea kufunga mabao mawili yaliyoipa ushindi huo. 
Alianza Domayo dakika ya 80 aliyefunga bao zuri kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la 18 akimalizia mpira uliotemwa vibaya na mabeki wa Kagera Sugar kabla ya Bocco kufunga la ushindi dakika sita baadaye akifunga kwa kichwa safi kufuatia krosi iliyochongwa na Shaaban Idd. 
Bao hilo linamfanya Bocco kufikisha mabao matano kwenye msimu huu wa ligi akizidiwa mabao mawili na Shiza Kichuya wa Simba, anayeongoza kileleni kwa mabao saba.

Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba
Timu zilivyokuwa zinaingia Uwanjani
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar
Kikosi cha Azam Fc
Kikosi cha Azam Fc kilichoanza dhidi ya Kagera Sugar leo kwenye Uwanja wa Kaitaba

Kikosi cha Azam Fc leo kilikuwa:
Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael/Khamis Mcha dk 79, Aggrey Morris, Daniel Amoah, Jean Mugiraneza/Frank Domayo dk 70, Ramadhan Singano, Salum Abubakar, John Bocco (C), Mudathir Yahya, Gonazo Ya Thomas/ Shaaban Idd dk 62

Ushindi huu pia ni wa pili mfululizo baada ya Timu ya Kagera kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Yanga kwa bao 6-2 na sasa Timu hiyo kupoteza pointi 3 mbele ya Azam Fc kwa bao 3-2. Kitendo kilichowafanya Mashabiki wa Kagera Sugar kuandamana wakionesha Mabango katika Mchezo huo.
Mashabiki wakiwa na Jazba kubwa Uwanjani Kaitaba
Mashabiki wa Kagera Sugar wakiwa na Mabango wakionesha ujumbe wao kwa Timu yao inayoongozwa na Maxime.
Wakidai kuwa ana Tabia ya kuuza Mechi.Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakijiuliza
Kagera Sugar wakiwa hoi baada ya Azam Fc kusawazisha bao kwa kufanya 2-2
John Bocco ‘Adebayor’ akigombea mpira wa kichwa
Kichapo cha pili mfululizo
Waamuzi wa Mtanange huo
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa na Ujumbe wao
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar
Juu kwa juu Wanahabri wa Azam Fc wakichukua Picha
Bocco tena
Penati.... mpira ukipangwa
- -