Makala : Mange Kimambi ni Nani? Kumbe kasoma Arusha? Na Jeff Msangi. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Mar 2017

Makala : Mange Kimambi ni Nani? Kumbe kasoma Arusha? Na Jeff Msangi.


By Jeff Msangi
Posted on February 27, 2011 

Kama wewe ni mfuatiliaji wa masuala ya watanzania mtandaoni,bila shaka utakubaliana nasi kwamba miongoni mwa mahali ambapo mengi hutokea na mengi huandikwa kama sio kujadiliwa basi mahali hapo ni katika blog inayokwenda kwa jina la U-turn.


Ni blog ambayo ingawa haina umri mkubwa(ilianzishwa mwaka mmoja na nusu tu uliopita), tayari imefanikiwa kuwa chanzo muhimu cha habari,michapo,maoni,matukio bila kusahau udaku wa hapa na pale.Ni mafanikio ambayo sio ya kubeza.It is what it is!


Mwendeshaji na mmiliki wa U-turn si mwingine bali Mange Kimambi ambaye miaka michache iliyopita ilikuwa ukisikia jina lake basi ilikuwa ni kupitia kurasa mbalimbali za magazeti hususani yale yanayoitwa “magazeti pendwa”. Leo hii mambo ni tofauti. Ni mama,mke,mwanafunzi na blogger mwenye idadi kubwa tu ya wasomaji na wafuatiliaji.


Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ya kina. Hii ni mara ya kwanza kwa Mange kufanya mahojiano ya kina na chombo chochote cha habari.


Je,Mange ni nani hasa?Ametokea wapi mpaka kufikia alipo hivi sasa ambapo kila siku idadi ya wasomaji na wanaofuatilia maisha yake na anachokiandika inazidi kuongezeka? Ni matukio gani katika maisha yake ambayo kwa namna moja au nyingine yamechangia in making her who she is today?


Nini siri ya mafanikio yake au ya blog yake?Unataka kujua ana maoni gani kuhusu mambo mbalimbali kama vile uongozi wa Rais Jakaya Kikwete?Ana ushauri gani kwa wasichana wadogo(teen girls)? Kwa majibu ya maswali hayo na mengine mengi,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;


BC: Mange,Karibu sana ndani ya BC.Mambo vipi?


MANGE: Asante sana.Feels good to be here!


BC:
Nimewahi kusoma mahali kwamba maisha yako ni kama vile kitabu kilicho wazi(an open book) ambapo kila anayetaka kusoma anayo nafasi ya kufanya hivyo.Lakini bila shaka utakubaliana nami kwamba wapo ambao hawajui lolote kuhusu historia ya maisha yako.Naomba tuanzie hapo…kwa kifupi tu ulizaliwa wapi,lini,ukasomea na kukulia wapi na mambo kama hayo.


MANGE: Nilizaliwa Hindu Mandal,Hospital- Dar es Salaam.Cheti changu cha kuzaliwa kina mwaka tofauti na passport yangu.According to my passport, I was born in 1980 lakini tukifuata Birth Certificate kuna difference ya 4years.Hii imetokana na kuna wakati mama yangu alitaka kunitoa kwa baba yangu akidai kwamba nina miaka chini ya 7.So kutokana na sheria za Tanzania natakiwa kuishi na mama. Baba yangu naye akawa na documents zake zinazosema nimeshapita miaka 7 kwa hiyo natakiwa kuishi na baba.So mama alikuwa na cheti changu cha kuzaliwa chenye umri tofauti na baba naye na passport yangu yenye umri tofauti.GO FIGURE.


Primary nilisoma Arusha School iliyoko Arusha- the best memories of my childhood came from my time there. Nilifanikiwa kufaulu mitihani ya darasa la 7 na nilichaguliwa kujiunga na Arusha Secondary.Baba yangu alifurahi sana na akanizawadia kwa kunipeleka kusoma Zimbambwe.So niliishi Harare miaka kadhaa kwa masomo yangu ya secondary.


Baada ya hapo nilikwenda Marekani kuanza masomo yangu ya juu.Kwa bahati nzuri (siwezi kusema bahati mbaya) nilijifungua mtoto wa kike,Bhoke, nikiwa Marekani jambo ambalo lilinifanya nirudi nyumbani kujipanga upya.


Then in 2004 nilijiunga na AVU-UDSM ambapo nilipata degree yangu ya Business Administration na sasa nipo Dubai nasoma Masters(MBA)


Mostly nimekulia Dar-es-salaam.


BC: Unakumbuka nini zaidi kuhusu maisha yako ya utotoni?Ulitaka kuwa nani,ulipenda michezo gani na tukio gani la utotoni ambalo hutokaa ulisahau?
MANGE: Yaani sijui pa kuanzia. Maisha yangu ya utotoni hayakuwa mazuri sana.,Mimi nimelelewa na baba yangu pamoja na mama yangu wa kambo. Baba alinipenda mno kama roho yake yote.Ila mama yangu wa kambo alinitesa sana.Niliishi maisha machungu sana enzi za utoto wangu. Huyu mama aliolewa na baba yangu nadhani kabla hata sijafikisha miaka miwili.Imagine mwanamke ukabidhiwe mtoto wa miaka miwili huyo mtoto si atadhani wewe ni mama yake?Ila mama yangu wa kambo alikuwa na roho mbaya sana.Alikuwa akinipiga sana,kunitukana sana,hanivalishi vizuri kama anavyowavalisha wanae.Alichokuwa akichukia zaidi ni mapenzi baba yangu aliyokuwa nayo kwangu. Ilifika stage nilikuwa nalilia kusoma boarding school ili tu niwe mbali naye.


Na kutokana na mateso niliyokuwa nayapata kwa mama yangu wa kambo, nilijikuta nimekuwa bully shuleni. Kwanza nilifukuzwa shule ya vidudu nikiwa na miaka 6 sababu ya kupiga watoto wa kihindi.Imagine miaka 6 nilifukuzwa shule!Primary nilisoma Arusha school, ambako huko ndo mpaka leo nina maadui sababu nilikuwa ni mwonevu sana.Nilikuwa napiga sana watoto wa wengine.Nilikuwa sisikii,nilikuwa mtoto mtukutu.


Baadaye nilikuja kuelewa kuwa hii yote ilitokana na mateso niliyokuwa napewa na mama yangu wa kambo nyumbani na ndio maana na mimi nilikuwa nikifika shule nawafanya watoto wengine kama mimi navyofanywa nyumbani kwetu.


Mama yangu wa kambo alikuwa ni mnyanyasaji sana wa wafanyakazi wa ndani. Nyumbani kwetu siku zote kulikuwa na vyakula vya aina mbili;chakula chetu cha familia na chakula cha wafanyakazi. Na wafanyakazi chakula chao ni ugali maharage au ugali na mchicha.Nyama wanakula mara moja kwa wiki,na wali pia wanakula mara moja kwa wiki.Ilikuwa inaniuma sana mpaka nikaanza tabia ya kupakua chakula kingiii ambacho siwezi kumaliza ili niwape angalau waonje.Yaani nilikuwa najiona na mimi nina hadhi kama ya wafanyakazi wetu kwa jinsi alivyokuwa akinichukia.Naamini angekuwa na uwezo hata mimi angekuwa akininyima chakula.


Leo hii ninavyoishi mimi,chakula ninachokula mimi ndicho anachokula mfanyakazi wangu.Hata siku moja sijawahi kumwambia ale tofauti na ninavyokula mimi.


Ila kwa upande mwingine yule mama kutokana na maisha magumu aliyonipa tangu nina miaka miwili mpaka nimekuwa mkubwa amenisaidia sana. Kutokana na yale mateso nilijifunza kuji-defend, nilijifunza kufight for myself na the biggest thing nilijifunza ni kwamba hata leo hii ningeolewa na mtoto mwenye mtoto asiye wa kwangu ningempenda huyo mtoto zaidi ya wa kwangu niliyemzaa.


KWA KWELI MY CHILDHOOD WAS THE WORSE PARTY OF MY LIFE,huwa sipendi hata kufikiria wala kukumbuka.Yule mwanamke aliniumiza sana,ila alisahau kwamba watu huwa wanakuja kuwa watu wazima na huwa hawasahau especially kama hujawahi hata kuomba msamaha kwa ulichofanya.


Kuhusu michezo;nilikuwa napenda michezo mingi sana. Nilipata bahati ya kwenda shule iliyokuwa inajali sana sports(Arusha School).Yani mimi ni nilikuwa kapteni wa michezo yote,swimming,kukimbia, na wakati na graduate nilipata tuzo ya sports girl of the year.


Tukio la utotoni ninalolikumbuka mpaka leo ni hili; nilisomaga Bunge Primary School kwa muda wa mwaka mmoja. Basi kuna wakati sikwenda shule kwa muda wa wiki 2 nilikuwa naenda kucheza. Baba yangu akapata taarifa siendi shule.Basi kesho yake akaenda na mimi mpaka shule, asubuhi wakati wa assembly akanichapa mbele ya shule nzima,yani viboko vya ukweli.Ilikuwa noma sana.


BC: Du,pole sana Mange. Kwa upande mwingine nilisikia kwamba wewe na mama yako wa kambo mnagombea mali za Marehemu Mzee Kimambi?Kuna ukweli katika hili?


MANGE: Sio ukweli, hatukuwa tukigombea.Ni kwamba tu baba yangu hakuacha will.So youu can imagine mtafaruko uliotokea hapo. Mimi niliridhia yeye awe msimamizi wa mirathi nikiamini kuwa atanipa kilicho changu.Ila nikaona muda unaenda sikabidhiwi share yangu ndio nikarudi mahakamani.


Anyways,mambo yanaenda vizuri tu sasa nimeshakabidhiwa mali kadhaa. Kabla ya mwisho wa mwaka tutakuwa tumeshamaliza makabidhiano.Shukrani nyingi zimwendee mwanasheria wangu Mama Tenga ambae alinipigania sana nipate share yangu na mpaka sasa bado ana fight on my behalf sababu mimi niko mbali.Mange and her daughter,Bhoke.


BC: Nakumbuka Mzee kimambi alikuwa anamiliki Tiger Motel na lile jumba kubwa la kifahari Mbezi Beach,je bado unaishi pale unapokuwa Tanzania? Na ile hotel imeuzwa au la?


MANGE: Mimi na familia yangu nzima tumeishi kwenye ile nyumba Mbezi Beach tangu mwaka 1989 tulivyohamia kutoka Temeke. Nikiwa Dar siishi pale na sijaishi pale zaidi ya mwaka mmoja sasa kutokana na kutoelewana na matatizo ya hapa na pale.Ila kisheria ile nyumba ina milikiwa na watu wanne wakiwa ni mimi,wadogo zangu wawili na step mother wangu na nina haki ya kuishi pale muda wowote nitakaojisikia.Hata watoto wangu wana haki ya kuishi pale. Same na Tiger Motel wote tumeshamegewa share zetu mahakamani sasa nasubiri tu kukabidhiwa mshiko wangu sababu shareholders waliobaki wanataka kuni buy out ila kama ikishindikana mimi nita wa buy out au hotel itapigwa mnada kila mtu apewe chake.Ni hayo tu.


Naomba usiniulize swali lingine linalohusu mirathi ya baba yangu.It’s a very sensitive issue, especially ukizingatia kwamba huyo mama yangu wa kambo pia ndo mama wa kaka zangu wawili ambao nawapenda kupita kiasi.So tuachie hapa hii issue.


BC: Kama binadamu huwa tunapewa ushauri au mawazo mbalimbali.Ni jukumu na maamuzi yetu kuyazingatia au kuachana nayo.Kwa upande wako unaweza kukumbuka ushauri gani ambao unadhani ulikuwa wa maana zaidi na ambao umeuzingatia mpaka leo katika kuendesha maisha yako.Nani alikupa ushauri huo?


MANGE: Ushauri mzuri sana niliowahi kuupata katika maisha yangu ni kuhusu elimu.Baba yangu alikuwa mkali sana kwenye suala la shule.Siku zote alikuwa akiniambia bila shule sitokaa kuheshimwa. Pia Dr. Mwele Malecela amekuwa akinishauri kuhusu suala la shule mpaka leo hii. Na naweza kusema huu ushauri umenisaidia sana kwenye maisha yangu kwani nina uhakika chochote kikitokea kwenye maisha yangu elimu yangu itanistiri.


Na baada ya baba yangu kufariki ghafla na kutuacha tukiwa hatujui tuanzie wapi, nilijifunza kwamba mwanamke hutakiwi kujiweka tu bila shughuli yoyote au elimu sababu umeolewa na mtu mwenye uwezo kwani huwezi kujua Mungu kapanga nini.Kwa hiyo ni lazima kujidhatiti na elimu.ELIMU ITAKUSTIRI.


BC: Ni kitu gani kilichokushawishi kuanzisha blog ya U-Turn na kwanini jina U-Turn?Malengo yako ya awali yalikuwa ni yapi? Bado malengo ni yale yale au yamebadilika kidogo?


MANGE: Ukweli ni kwamba kitu kikubwa kilichonifanya nianzishe U-TURN ni baada ya kuona nanyanyasika sana kwenye magazeti ya udaku na blog za watu wengine.Yani magazeti ya udaku –ya Eric Shigongo yalikuwa yanaandika mambo mengi sana ya uongo juu yangu na nilikuwa sina pa kwenda kuelezea upande wangu.Au sometimes nilikuwa nafungua blog ya mtu nakuta comments kuhusu mimi halafu nakuwa sina jinsi ya kujitetea.Kusema ukweli this was the biggest motivation, I JUST WANTED TO BE HEARD.


At first lengo la u-turn lilikuwa ni ku-entertain watu,watu wenyewe wakiwa ni the younger generation 18-40yrs old,na mpaka leo lengo bado ni hilo hilo.


Jina U-TURN nilichagua kutokana na neno lenyewe u-turn.I believe in second chances in life; kwamba unapoona unaelekea kusiko and you wish to make a u-turn uanze upya you can always do so.


BC: Umekuwa blogger kwa muda sasa.Unaweza kusema blogging imebadilisha maisha yako kwa njia moja au nyingine?Kivipi?


MANGE: Mpaka sasa nimekuwa nikiblog kwa muda wa mwaka mmoja na mienzi 6 hivi.Yaani blogging imebadilisha maisha yangu.Before blogging wengi walikuwa wananijua coz of magazeti ya udaku na blog zingine.Ila baada ya mimi mwenyewe kuanza kublog,sidhani kama kuna mtu hanijui…lol….which in a way is great coz message zangu zinakuwa zinawafikia watu wengi sana.


Kwa upande mwingine ni mbaya kwa sababu sasa kuna wasichana wengi wadogo wanapenda kufanya vitu navyofanya,au kuvaa ninavyovaa na mambo kama hayo.In short wanani-admire so hiyo no pressure kubwa kwangu sababu inanibidi niwa influence positively.


BC: Je,kuna siku iliwahi kutokea ukatamani kuachana na blogging?Kama ndio,ilikuwaje?


MANGE: Yes, kuna wakati mwaka jana nilitaka kuacha kublog kutokana na ambitions zangu nilizonazo for the future.Washauri wangu wakaniambia kama kweli nataka hicho kitu niachane na kublog huku wengine wakiniambia nisiachane na u-turn coz naweza kuihitaji huko mbele.


Pia mwaka jana mwishoni nilitaka kuacha sababu ya shule na kuwa na mtoto mchanga. Na nilishaacha ila wasomaji wangu walinisihi sana nisiache wakidai washakuwa addicted to u-turn.My readers are amazing….


BC: Blog yako imekuwa ikitupiwa lawama mbalimbali.Lawama kubwa ni kwamba imekuwa ikitumika kama sehemu ya watu kutukanana,kusengenyana na mambo kama hayo.Nini msimamo wako kama mwendeshaji na mmiliki rasmi wa U-Turn.


MANGE: Unajua mimi ni mtu niliye wazi sana. Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa uturn utaona kwamba mie huwa naachia comments za watu hata wanapokuwa wananinanga mimi mweneywe.That’s because I believe in freedom of speech.Ila ni kweli naona inabidi nichuje kidogo posts za uturn na comments ambazo zinasengenya watu sababu nia yangu sio kumfedhehesha yeyote.Mange with one of her best friend,Mwamvita Makamba


BC: Kuna maneno kwamba wewe huelewani na bloggers wenzako hususani wa kike. Kuna ukweli wowote katika hilo? Kama sio unadhani nini kinachangia kuenea kwa tuhuma kama hizo?


MANGE: Ha ha ha, unajua mimi ni mtu tofauti sana.Mimi ni mtu ambaye ni rahisi sana mtu kumpenda na pia ni rahisi sana mtu kunichukia tena bila sababu.Kuna wengi hawanipendi halafu hawajawahi hata kuniona,meaning hawanijui,nina damu ya kunguni tu.lol


Kuhusu hao bloggers wa kike,I guess unayemuongelea ni TK.TK kaokoka these days.So her being the God fearing person that she is, she got in touch with me na kwa muda wetu,privately bila kumuhusisha yeyote tumeyamaliza matatizo yetu recently.


Blogger yeyote mwingine wa kike mwenye matatizo na mimi ni wivu tu unamsumbua.Si unajua wanawake jinsi hatupendani na kuoneana wivu bila mpango.Most bloggers wamekuwa around kabla yangu,halafu mie nikaanza tu ghafla nikawafunika basi ndo imekuwa issue.Manake ukiwauliza Mange kakufanya nini sidhani kama utapewa jibu la msingi.


BC: Blog yako inatembelewa na watu wangapi kwa siku na unatumia muda kiasi gani kwa siku katika kuandika,publishing,kukagua maoni na vitu kama hivyo?


MANGE: Siku za weekdays, kwa siku U-turn in hits kati ya 5000-8000.


Siku za weekends hits ni kati ya 2000-4000. Yani wasomani wangu wanapenda sana kutuma comments.Natumia muda mrefu mno kusoma comments ili nijue zipi niachie,sometimes nachoka kuzisoma na bahati mbaya nakuwa naachia comments zisizofaa.Kwa siku natumia kama 3hrs hivi kutafuta materials za kupost.


BC: Bila shaka umewahi kuzisikia hizi shutuma kwani nakumbuka umewahi kuziongelea; kwamba blog yako au maisha yako una=promote kwamba kuolewa na mzungu ndio njia mbadala au ya kisasa kwa wasichana wa kitanzania endapo wanahitaji kuwa na maisha mazuri.Unajisikiaje unaposikia tuhuma kama hizo?


MANGE: Yani hii issue inaniumiza sana.Sijui hata imetokea wapi.Hivi watu wamesahau nina mtoto wa kike anayeitwa Bhoke na baba yake ni Mtanzania?Sasa leo kwanini niseme kuolewa na mzungu ndio the only way?Labda wanahisi kama ningeolewa na mweusi nisingeweka maisha yangu hadharani.Ukweli ni kwamba I’m such a free spirit na chochote nachofanya sasa hivi ningefanya hata kama ningeolewa na mbongo mwenzangu.


Halafu nani kasema kuolewa na mzungu ndio kuwa na maisha mazuri? Mbona nawajua watu wengi sana walioolewa na wazungu na wamefulia tu? Na kuna wengi nawajua wameolewa na weusi na wako juu ile mbaya? Na pia kuna wanawake nawajua hata kuolewa hawajaolewa na maisha yao ni babkubwa.Na wengine wako divorced na maisha yao ndio yamezidi kushamiri.


Kuolewa na mzungu wala mweusi si chochote.Mwanamke wa maana ni yule ambaye siku yoyote anaweza kuishi bila mwanaume na maisha yake yakawa babkubwa.Mange,her husband and son,Kenzo.


BC: Pamoja na ku-blog,wewe ni mfuatiliaji wa masuala mbalimbali ya siasa za Tanzania.Bila kuficha umekuwa ukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi(CCM).Ni mambo gani ya kiutendaji na kiutawala ambayo yanakuvutia zaidi katika CCM ambayo huyaoni katika vyama vingine? Unauzungumziaje uongozi wa Rais Jakaya Kikwete?


MANGE: Mimi ni mtoto wa CCM.CCM ni kila kitu kwangu.Bila CCM labda nisingekuwa hapa nilipo.Baba yangu alikuwa supporter mkubwa wa CCM.So toka utotoni nimelelewa nikiona wazazi wangu wakikipenda Chama Cha Mapinduzi.Of course na mimi hakuna kingine ninachokijua zaidi ya CCM.


Mambo ya kiutendaji yanayonivutia ni kuhusu suala zima la udini.Hivi umenotice kwamba CCM has an unwritten law kwamba lazima marais wanakuwa wanapokezana kutokana na dini? This time Rais akiwa Mkristo basi atakayefuata atakuwa Muislam.That way watanzania wanakuwa united.Pia angalia bara la Africa ni nchi ngapi Africa zinaweza kujivunia amani kama Tanzania? CCM ni chama chenye nguvu,chama cha haki,chama cha wananchi.


Nilipata bahati ya kumfahamu vizuri Rais Jakaya toka nina umri mdogo sana.I have watched him climb the political ladder toka enzi hizo. Ukweli ni kwamba JK ni Rais mwenye charisma na ndio maana watanzania wengi walimpenda sana na waliweka imani zao nyingi kwake wakati anaingia Ikulu.


Ila sijui nini kilitokea hapo kati kati akajikuta kazungukwa na mafisadi, na ameweka rekodi ya Mgombea wa CCM aliyeshinda kwa kura ndogo sana.Hii yote inatokana na kwamba watanzania wengi walipoteza imani nae kutokana na zile tuhumu za ufisadi zilizotokea ndani ya baraza lake la mawaziri hapo kati kati.Ila kwa hiki kipindi chake cha pili kwa kweli kajitahidi sana na baraza lake la mawaziri.Tumeona new faces ,na old faces zilizorudi ni watu wanaopiga kazi kweli kweki kama Magufuli,Mwakyembe,Nyalandu etc.


Unajua Tanzania ni nchi yenye potential sana.At the moment kuna matatizo kidogo ya utendaji kwenye uongozi mzima wa nchi na watu wenye uchu wa madaraka kama CHADEMA wanatumia matatizo tuliyonayo sasa hivi kuwadanganya wananchi kwamba CHADEMA ndio suluhisho.


Watanzania nina hili la kuwaambia siku mtakayo wakabidhi CHADEMA nchi yetu,labda mtakuwa na umeme kwenye majumba yenu,ila pia tutakuwa tunalala tukisikia sauti za mitutu ya bunduki next door.


Kwanini wewe kama mtanzania unayelalamika kuwa CCM hawaiongozi nchi vizuri kwanini wewe usiende kugombea ubunge huko CCM,au nyadhifa yoyote serikalini ili ubadilishe mambo? Mbona kuna vijana wengi mwaka jana wamegombea na wameingia mjengoni,kama January Makamba. Kuliko kukaa na kulaumu jiulize na wewe unaifanyia nini nchi yako,CHADEMA,NCCR MAGEUZI,CUF na upinzani mwingine wowote sio solution.Solution ni sisi wenyewe na sio kukabidhi nchi yetu watu wasio na experience, au chama kichanga kilichojaa wauza sura. BE WARNED MTANZANIA.


BC: Sasa tuongelee kidogo kuhusiana na masuala ya urembo na fashion kwani ni wazi kwamba mambo hayo unayapa kipaumbele.Ni designer gani unayempenda zaidi au ambaye unavaa vitu vyake zaidi?


MANGE: Mie sivai designer kaka yangu.Natengeneza college fund za watoto ,retirement funds na nyumba.


Mie navaa nguo kutoka duka lolote lenye hadhi ya kati kati kama vile Zara,Jane Norman,River Island,Bebe,Oasis,Top Shop, H&M, Forever 21,KIKIS FASHION etc.


The only thing lazima nivae disigner ni sunglasses tu.Ila tukiongelea designer anayenivutia kwa nyumbani ni Ally Rhemtullah na Mustafa Hassanali.Kwa mamtoni ni Oscar de la Renta.Mange(right) with some of her best friends


BC: Ni vitu gani vya urembo ambavyo ni never miss katika pochi yako unapotoka?


MANGE: My Mac face powder,Clarin lip gloss,hair brush,Driving licence ,cash & MY BLACKBERRY.


BC: Wewe ni mke,mama,mwanafunzi(pursuing MBA),blogger,shangazi,Ndugu nk.Unawezaje kuoanisha au ku-balance mambo yote haya kwa mpigo?


MANGE: Yani ni ngumu sana.Sababu nawapenda wote walio kwenye maisha yangu na pia napenda kusoma na kuwa na elimu.So nimetafuta jinsi ya kujigawa .Hubby akiwa busy na drawings zake na mie nablog.Mchana akiwa kazini nakuwa busy kusoma au kwenda class na kucheza na mwanangu,Kenzo.


Also natafuta muda wa kuchat na ndugu,jamaa na marafiki kwenye blackberry yangu.I’m addicted to my phone.Weekends siblog kabisa.Weekend ni muda wa kuspend time na mume wangu na mtoto wangu na sometimes going out with friends.Mange’s husband with their son,Kenzo.


BC: Nikikupa nafasi ya kuwapa ushauri wasichana wadogo(teen girls),ungependa kuwapa ushauri gani?


MANGE: Ningependa kuwashauri kwamba ELIMU ni ufunguo wa maisha.Pia ningependa kuwaambia kwamba, wawe wajasiri wa kuongea wanachotaka kuongea bila woga.Na wawe wakijiamini na kujipenda wenyewe.Wasisikilize yoyote anayewaambia hawawezi kufika mbali au kufanya hiki au kile.In life there will always be people to discourage you.Just be strong.


BC:
Nini mipango yako kimaisha,kiutendaji na uwajibikaji katika miaka 5 ijayo?Will the U-Turn phenomena remain alive?


MANGE:
Yani nina ndoto nyingi sana.Muda mwingine silali usiku nawaza vitu navyotaka kufanya na maisha yangu.Nashukuru Mungu nimepata mume ambae hanibani na anayenishawishi kufuata dreams zangu.


Kuna kitu kikubwa sana napanga kufanya 2015.Nikiwa tayari nitakiweka wazi kwa mdomo wangu mwenyewe.Ndani ya miaka 5 ijayo nataka kutumia umaarufu nilioupata kupitia U-turn kuwasaidia wanaohitaji msaada wangu.Nataka kuonyesha watu kuwa kuna side nyingine ya Mange kimambi ambayo ni kuwa humble and caring.


Nategemea kuitumia MBA yangu kupata misaada ya kuwasaidia wanaohitaji msaada.In short I want to give back to the county that has given me so much.


U-TURN ipo kwa sasa, inaweza ikawepo ndani ya miaka mi5 ijayo au labda kuna siku tutaamka asubuhi na kukuta haipo hewani.Lets enjoy it while it lasts.lol…
BC:
Asante sana Mange kwa muda wako.Kila la kheri katika kazi zako.
MANGE: Asanteni pia na endeleeni na kazi nzuri mnayofanya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad