Shule 10 Bora Jijini Arusha : Shule ya Msingi ya HADY Primary School Yafanya Vizuri katika Mitihani ya Darasa la Saba 2015 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Nov 2015

Shule 10 Bora Jijini Arusha : Shule ya Msingi ya HADY Primary School Yafanya Vizuri katika Mitihani ya Darasa la Saba 2015

Shule ya Msingi Hady Nursery and Primary School iliyopo Sombetini, Jijini Arusha imekuwa miongoni mwa shule bora zilizofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba, uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu kote nchini.

Katika Matokeo yaliyotangazwa Mwishoni mwa wiki iliopita na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini NECTA Dk.Charles Msonde, ufaulu wa Kitaifa mwaka huu umepanda kwa asilimia 10.85 kutoka asilimia 56.99 za mwaka jana, ambapo wanafunzi waliofaulu ni 518,034 kati ya 775,273 waliosahiliwa mwaka huu.

Kwa upande wa Matokeo ya Shule ya HADY , Matokeo yanaonyesha kuwa shule hiyo imeshika nafasi ya Pili (2) kati ya shule 106 katika Wilaya ya Arusha Mjini, nafasi ya Sita (6) kati ya shule 603 katika Mkoa wa Arusha na nafasi ya 136 kati ya shule 16,096 Kitaifa.



Wahitimu wote 109 wa shule hiyo wakiwemo wa kiume ni 58 na wa kike 51 wamefaulu mtihani wao kwa madaraja yote ya ufaulu jambo lililofanya shule hiyo kupokea pongezi mbalimbali kutoka kwa wazazi na walezi wa wahitimu hao kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.

BOFYA JINA LA SHULE HAPO CHINI ;UPATE MATOKEO YA SHULE KUMI BORA KWA WILAYA YA ARUSHA

1.Upendo Friends Primary School

2. Hady Primary School 

3. Nalopa Primary School

4. Green Valley Primary School

5. Ghati Memorial Primary School

6. St. Jude Primary School

7. Arusha Alliance Primary School

8. St. Monica Primary School

9. Imani Primary School

10. Mecson Primary School  

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad