Na Woinde Shizza, Kilimanjaro
Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umemtaka Waziri
mstaafu Frederick Sumaye hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza
kumfanya awe na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika
uendeshaji wa serikali na masuala ya utawala.
Sumaye ametakiwa amuache Rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwasababu alipewa dhamana
ya kuwa Waziri mkuu lakini hajufikia hata thukuth ya utendaji
unaofanyika sasa.
Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu katibu mkuu wa uvccm
shaka hamdu shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa ccm wa kata
mbili za kwandele na mbichi jimbo Rombo mkoani kilimanjaro.
Shaka alisema anachokifajya sumaye na baadhi ya wanasiasa
muflis wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu
ya tano ni kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa
madarakani wananchi wameyasahau.
Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu
katika utendaji na usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais
hakuna atakayempita Sumaye.
"Amekuwa waziri mkuu kwa miaka kumi kuliko waziri mkuu
yeyote na kwa bahari mbaya sana ndiye waziri mkuu zero kuliko mwingine
yeyote tokea tupate uhuru mwaka 1961 "alisema shaka.
Aidha Kaimu huyo katibu mkuu alimuonya sumaye akimtaka
aache kumfuatafuata Dk Magufuli katika mikakati yake ya kutumikia nchi
na juhudi anazichukua dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma
nchini.
Alisema wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na
nia ya wazi iuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima
alisema kina sumaye na wenzake wafumbe midomo yao na waache mara moja
kumbughudhi Rais kwa ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa.
"Sumaye aacha kufuatafuata Rais na kujifanya unajua wakati
mambo yalikushinda wakati ukiwa PM, kama huna maneno ya kusema rudi
Hanang ukalime maharage na karanga "alisema
Pia shaka aliwataka wananchi wa jinbo la Rombo
kujitatayarisha ili kumpiga chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya
chadema Joseph Selasini kwasabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia
wananchi wa jimbo hilo.
"Siku zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika,
selasimi hajui anavhokufanya wala hajali shida na matatizo yaliopo
katika jimbo lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisotiza
shaka
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa
kilimanjaro Juma Raib Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini
kuacha mara moja tabia ya kushiriki na kuchagua vyama na wagonbea wa
nafasi mbali mbali kwa ukabila, ujimbo au nasaba.
Raibu alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi
katika Mikao yote ya Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni
wabaguzi kwa misingi ya asili au ujamaa.
"Tunachotaka kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya
Kaskazini ni kumuasi baba wa Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere,
haiutuacha tukiwa tumegawahyika , tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa
ukabila au udini, chadema acheni kwasabahu hilo ni baa au janga katika
jamii "alisema Raib.
Jumla ya wananchi wapya 103 wa ccm na jumiya zake
walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka alipata nafasi ya kuangalia
mechi ya soka kati ya timu za kata za makiidi na mahare wilaya Rombo.
No comments:
Post a Comment