Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeingia makubaliano na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ili kubadilishana taarifa na kusomana mifumo ya kudhibiti mapato yatokanayo na wasanii, na pia kubaini wasanii wanaolipa na wasiokodi.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Desemba 24, 2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Yusuph Mwenda mifumo hiyo itaweza kubaini na kutambua ni wasanii gani na wangapi wanaolipa na wasiolipa kodi.
Aidha amesema kuwa kuna wasanii watapata kiasi kikubwa cha fedha kupitia kazi yao, hivyo kuna umuhimu na wao wakalichangia taifa kupitia kulipa kodi lakini pia kodi watakayoitoa ni ndogo na haitambana ashindwe kulipa kodi.
"Msanii atakayekuwa na mapato ya chini ya 170,000 Serikali imemsamehe, atakayekuwa na mapato yatakayozidi hapo atachangia kiasi kidogo, Msanii atakayeanzisha kampuni yake akiwa na mapato chini ya Milion.4 kwa mwezi atasamehewa kulipa kodi lakini akiwa na mapato kwa mwaka kuanzia Mil.7 atachangia laki moja kwa mwezi, na yule atakayekuwa na mapato ya Sh. Mil.7 hadi Mil. 11 atalipa laki mbili na nusu kwa mwezi (250,000) akiwa na mapato kuanzia Mil. 11 hadi 100 kwa mwezi atachangia asilimia tatu na nusu ya kile anachoingiza". Amesema
Pamoja na hayo Kamishina Mwenda amesema kuwa, makubaliano hayo itawezesha kusomana mifumo kati ya TRA na BASATA katika ukuzaji na kuendeleza sekta ya sanaa nchini.
Amesema hiyo ni katika utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kutaka taasisi, makampuni za umma na kusomana kwa mifumo na taarifa.
Nae Katibu Mtendaji BASATA, Dkt. Kedmon Mapana amesema hii mifumo inakwenda kuleta mapinduzi na mabadiliko makubwa katika sekta ya sanaa kwa wasanii wote wakiwemo waimbaji, wachoraji, MC, wachongaji na wengine ambao wanaingia kwenye sekta ya sanaa.
Amesema watakwenda kuipa Serikali muamko ya kuisaidia sekta hii kwakuwa wasanii wanalipa kodi ikiwemo mifumo itaenda kusaidia wasaniii na wadau wa sanaa kufanya shughuli zao bila bughudha yoyote kwakuwa mifumo inasomana.
No comments:
Post a Comment