Matukio : Taswira mbalimbali, waliohudhuria kongamano la DICOTA 2016 Dallas, Texas Marekani - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


29 Apr 2016

Matukio : Taswira mbalimbali, waliohudhuria kongamano la DICOTA 2016 Dallas, Texas Marekani


 Kutoka kushoto ni DariaMwakaramba kutoka Tanzania, Asya Idarous Khamsin toka Tanzania/Houston na Flora toka North Carolina ambao siku ya Ijumaa April 29, 2016 wataitikisa kongamano la DICOTA 2016 jijini Dallas kwa vivazi vya kukata na shoka kutoka Tanzania na hapa Marekani.
Wanamitindo wakiwa katika picha ya pamoja.
Kulia ni Mhe. Balozi Wilson Masilingi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na mkewe Marystela Masilingi (Wanne toka kushoto) wakimkaribisha Balozi Anisa Mbega  (wapili toka kushoto) anayeshughulikia maswala ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa siku ya Alhamisi April 28, 2016 katika hotel ya Hyatt Regency ambako ndiko litakapofanyika Kongamano la DICOTA 2016 kuanzia siku ya Ijumaa April 29, 2016.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani akisalimiana na ujumbe ulioongozana na Balozi Anisa Mbega (hayupo pichani) anayeshughulikia maswala ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa siku ya Alhamisi April 28, 2016 katika hotel ya Hyatt Regency ambako ndiko litakapofanyika Kongamano la DICOTA 2016 kuanzia siku ya Ijumaa April 29, 2016.
Kutoka kushoto ni Nasibu Sareva, Fredrick Mjema, Asha Nyang'anyi, Balozi Anisa Mbega, Mohamed Nuh mwakilishi wa People's Bank of Zanzibar, Emmanuel Kimaryo mwakilishi kutoka CRDB na Lunda Asumani wakiwasili katika hotel ya Hyatt Regency siku ya Alhamisi April 28, 2016.
Uhakiki wa majina ukiendelea.
 Dkt. Allen Rwabutaza kutoka Columbus, Ohio akiwa nje ya hotel ya Hyatt Regency mara tu baada ya kuwasili kwa ajili ya kongamano la DICOTA.
Jackson Munuo kutoka Massachusetts akiwa tayari kwa kongamano la DICOTA 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad