Afya zetu: Waziri Ummy Mwalimu atembelea Muhimbili na kukagua utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Feb 2016

Afya zetu: Waziri Ummy Mwalimu atembelea Muhimbili na kukagua utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli linatekelezwa mara moja.
FSA_6533

Picha mbalimbali zinaonesha Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli pamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

FSA_6416 FSA_6443
????????????????????????????????????
FSA_6540
????????????????????????????????????

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad