Elimu :Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin SAUT 2016 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 13 December 2016

Elimu :Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin SAUT 2016

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin SAUT, Padri, Dkt.Thadeus Mkamwa (kushoto), akitoa taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Disemba 16 na Jumamosi Disemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza.

Kulia ni Bernald James ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi.

Wahitimu 2421 wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada, shahada za uzamili na uzamivu katika mahafali hayo huku wanafunzi wanafunzi 746 wakishindwa kutunukiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutolipia ada.

Mahafali hayo yatatanguliwa na Siku ya Jamii itakayofanyika Jumatano Disemba 14 ambapo kutakuwa na Maonesho ya Kitaaluma.
BMGHabari

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin SAUT, Padri, Dkt.Thadeus Mkamwa (kushoto), akitoa taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Disemba 16 na Jumamosi Disemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza.

Bernald James ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.

Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Disemba 16 na Jumamosi Disemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza.

Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho

Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho

Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT

Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho

Baadhi ya wajumbe wa baraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho

Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho

Wanahabari na wajumbe wa baraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho

Wahitimu 2421 wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada, shahada za uzamili na uzamivu katika mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine SAUT cha Jijini Mwanza.

Makamu Mkuu wa chuo hicho Dkt.Thadeus Mkamwa amesema wahitimu hao wakiwemo watatu wa shahada za uzamivu watatunukiwa shahada zao kwenye Mahafali yatakayofanyika ijumaa na jumamosi wiki hii chuoni hapo.

Amesema mahafali hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi yatatanguliwa na Siku ya Maonesho Kitaaluma yatakayohusisha wanafunzi na wahadhiri kutoka kila kitivo na idara.

Hata hivyo Dkt.Mkamwa amesema wanafunzi 746 wameshindwa kuhitimu masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kulipa ada.