HALI YA HEWA :MH. BENDERA AFUNGUA WARSHA YA SIKU MBILI YA WAANDISHI WA HABARI INAYOHUSU UMUHIMU WA UTOAJI TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA UMMA,MKOANI MOROGORO - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 3 September 2014

HALI YA HEWA :MH. BENDERA AFUNGUA WARSHA YA SIKU MBILI YA WAANDISHI WA HABARI INAYOHUSU UMUHIMU WA UTOAJI TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA UMMA,MKOANI MOROGORO


 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Warsha ya siku mbili ya Waandishi wa Habari ilinayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma,inayofanyika kwenye hoteli ya Oasis mjini Morogoro.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi na kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa.
 Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa akizungumza machache wakati akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na kwa washiriki wa warsha hiyo inayoendelea kufanyika hivi sasa kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Oasis,Mkoani Morogoro.
  Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa akizungumza jambo wakati akichangia moja ya mada zinazoendelea kuwasilishwa kwenye warsha hiyo inayoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Oasis,Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi akisisitiza jambo wakati akijubu moja ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya Wanahabari inayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,inayohusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mada mbali mbali zinazoendelea kuwasilishwa kwenye warsha hiyo.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya Wanahabari inayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma wakifatilia kwa makini mada zinazoendelea kutolewa kwenye warsha hiyo.
 Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment