Mkuu
wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Tarakea, wilayani Rombo Mkoa wa
Kilimanjaro, John Kapembe akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa
kiraia) eneo la Tanzania katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya.
Rwegasira yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akitembelea vituo vya
Uhamiaji vya mipakani mkoani humo.

Kaimu
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akimkaribisha Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (katikati meza kuu) azungumze na Maafisa wa Idara ya
mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha
Huduma Mipakani Holili wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Rwegasira
aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea
maendeleo nchi yao.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (katikati meza kuu) akizungumza na Maafisa wa Idara ya
mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha
Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Meja
Jenerali Rwegasira katika hotuba yake aliwataka maafisa hao wafanye kazi
kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.
Kaimu
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Holili, Edwin Mwasota akimuonyesha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (watatu kulia) moja ya ofisi zilizopo katika Jengo la Kituo
cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa
Kilimanjaro. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Victoria Lembeli. Meja Jenerali Rwegasira alifanya ziara ya kikazi kwa
kutembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani Kilimanjaro.
Afisa
Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku
(kushoto) akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto) mpaka Tanzania pamoja
na Jengo la Uhamiaji la nchini Kenya (Taveta) wakati walipokuwa juu ya
ghorofa ya Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili,
wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) akiondoka katika Jengo la
Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa
Kilimanjaro mara baada ya kumaliza ziara yake ya kulitembelea jengo hilo
na kuzungumza na maafisa mbalimbali wa serikali wanaotoa huduma za
mpakani mkoani humo. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa
Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku na Kulia ni Afisa wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpakani Holili, Aden Mwakalobo.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment