Malkia
wa Swaziland Mheshimwa Nomsa Matsebula akisalimiana na Mkuu wa Wilaya
ya Rufiji Ndugu Nurdin Babu mara baada ya helikopta iliyomchukua kutua
kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyamisati huko wilayani Rufiji
ambako alikwenda kutembelea Shule ya Wamanakayama inayomilikiwa na
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA. Tarehe 2.7.2014. Kulia ni Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.
Mke
wa Mfalme Mswati III wa Swaziland Malkia Nomsa Matsebula akisalimiana
na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wamanakayama Dkt.
Ramadhan Dau mara baada ya mgeni huyo kuwasili huko Nyamisati
Malkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwa amefuatana na mwenyeji wa Mama Salma
Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Nyamisati waliofika kumlaki
mara baada ya helikopta iliyomleta kutua kwenye uwanja wa Shule ya
Sekondari ya Nyamisati
alkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula akionyeshwa namna wanavyotumia I-pad
katika baadhi ya masomo yao hapo shuleni Wamanakayama na mwanafuzi
Rehema Shao aneyesoma kidato cha pili huko mwanafunzi Asia Idd (kushoto)
akisubiri zamu yake.
Mwanafunzi
Assia Idd akimwonyesha Malkia Matsebula kutoka Swaziland namna ya
kutumia i-pad kwenye masomo ya sayansi na hesabu wakati Malkia huyo
alipotembele Shule ya Sekondari ya Wamanakayama inayomilikiwa na Taasisi
ya WAMA inayoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na mgeni wake Malkia wa Swaziland
Nomsa Matsebula wakitembelea maeneo mbalimbali ya shule ya Wamanakayama
Mwanafunzi
Elizabeth Kipoto anayesoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya
wasichana ya Wamanakayama akiwaonyesha wageni jaribio la kujua kama
kuna protini kwenye vyakula katika maabala ya Biologia shuleni hapo
Malkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula akipanda mti wa kumbukumbu ya kutembelea
Shule ya Sekondari ya Wasichana Wamanakayama iliyoko katika Kijiji cha
Nyamisati katika wilaya ya Rufiji.
Mgeni akipanda mti
Wimbo wa taifa
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha Mgeni
wake Malkia Matsebula wa Swaziland kuongea na wanafunzi na wafanyakazi
wa Shule hiyo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha Mgeni
wake Malkia Matsebula wa Swaziland kuongea na wanafunzi na wafanyakazi
wa Shule hiyo.
Malkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Wasichana Wamanakayama baada ya kuitembelea shule hiyo
Malkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Wasichana Wamanakayama baada ya kuitembelea shule hiyo
Malkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Wasichana Wamanakayama baada ya kuitembelea shule hiyo
Malkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwa na mwenyeji wake Mama Salma Kikwete
katika picha ya pamoja na wanafunzi na viongozi mbalimbali.
Mke wa Mama Salma Kikwete akimpokea Mgeni wake Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebulan wakiongea na wanahabari
Mke
wa Mama Salma Kikwete akimpokea Mgeni wake Malkia wa Swaziland Nomsa
Matsebula mbele ya jengo la ofisi ya Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo,WAMA.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake
Malkia Nomsa Matsebula na Mama Hulda Kibacha, Mjumbe wa Bodi ya WAMA
(Kulia kwa Malkia), na His Royal Highness Prince Muvela (kulia) na His
Royal Highness Prince Sicalo (kushoto).
Malkia
Matsebula na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza Afisa Uragibishi na
Mawasiliano wa WAMA Ndugu Philomena Marijani akitoa maelezo juu ya kazi
mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi mgeni wake zawadi ya picha.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Malkia Matsebula zawadi ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa hapa Tanzania.
Malkia Nomsa Matsebula akimkabidhi Mama Salma Kikwete mchango wake wa dola 3000 kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Wamanakayama.
Malkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula akizungumza na Mama Anna Mkapa wakati wa
futari ambayo iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete huko Ikulu
Mama
Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa futari aliyomwandalia Malkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula anayetembelea Tanzania huko Ikulu
Malkia
wa Swaziland Nomsa Matsebula akiongea na viongozi wanawake mbambali
waliohudhuria futari aliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
huko Ikulu. PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment