Kaimu
Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto),
akimkabidhi, Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris
Semkiwa (kulia), bati na rangi zenye thamani ya sh.milioni 3.5
zilizotolewa na mfuko huo jana, kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule
ya Sekondari ya Mihande ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya
Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na
maabara. Anayeshuhudia makabidhiano hayo katikati ni Mkuu wa shule hiyo,
Flora Masha.
Hapa ni kubadilishana mawazo baada ya makabidhiano hayo.
Jengo la maabara la shule hiyo lililokamilika ujenzi wake.
Jengo la maabara ambalo ujenzi wake unaendelea.
Baadhi ya majengo ya shule hiyo yanvyoonekana.
Jengo la utawala la shule hiyo.
Dotto Mwaibale
MFUKO
wa Pensheni wa LAPF umeunga jitihada za Rais Jakaya Kikwete za
kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara kwa kutoa
vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh.milioni 3.5 kwa ajili ya kusaidia
ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande iliyopo
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mlandizi wilayani humo jana,
Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki wa mfuko huo, Isaya Mwakifulefule
alisema mfuko huo umejiwekea utaratibu wa kusaidia kutoa misaada
mbalimbali katika shughuli za maendeleo ya kijamii.
"Mfuko
wetu kila kanda nchini wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali
za maendeleo na katika hilo mnaweza kuwa mashuhuda kwani siku za hivi
karibuni mmeweza kuona tulivyotoa msaada kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa
ngozi (albino)" alisema Mwakifulefule.
Alisema
ujenzi maabara katika shule hapa nchini ni muhimu sana katika wakati
huu wa ulimwengu wa sayansi na teknolojia ambapo wanahitaji wanayansi
wengi kwa utaalamu wa aina mbalimbali hasa katika masuala ya utafiti.
Alitaja
vifaa vilivyotolewa na mfuko huo kuwa ni mabati na rangi kwa ajili ya
kukamilishia ujenzi wa maabara hizo na alitoa mwito kwa wadau wa
maendeleo na mifuko mingine kujitokeza kusaidia eneo hilo kwani kuna
mahitaji makubwa ya maabara nchini.
Akipokea
msaada huo kwa niana ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Ofisa Elimu
Vifaa na Takwimu wa wilaya hiyo, Doris Semkiwa alisema msaada huo
utapunguza changamoto ya ujenzi wa maabara kwenye shule hiyo.
Alisema
ujenzi wa maabara katika wilaya hiyo umekamilika kwa asilimia 67 na
kuwa ujenzi huo unaendelea kwa kasi ambapo wanatarajia kukamilisha kazi
hiyo mapema iwezekanavyo.
Alisema
kwa wilaya nzima yenye shule za sekondari 8 mahitaji ni kuwa na maabara
24 na tayari wamejenga 14 na kuwa fedha zinazotumika kwa ujenzi huo
zinatoka katika mapato ya ndani ya Halmshauri, wadau mbalimbali na nguvu
za wananchi.
Aliongeza
kuwa ujenzi huo utagharimu zaidi ya sh, milioni 400 na kuwa changamoto
kubwa ni mapato ya ndani kuwa kiduchu na kuwa kama wangekuwa na fedha za
kutosha wangeweza kumaliza kwa wakati ujenzi huo.
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha aliwashuku LAPF kwa msaada huo pamoja
na Halmsahauri kwa fedha za luzuku inazozitoa kila mwezi kusaidia mambo
mbalimbali katika shule hiyo na zingine sanjari na ujenzi wa maabara
hizo.
No comments:
Post a Comment