Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo wa Jimbo la Moshi Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Philemone Ndesamburo amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya KCMC, Mkoani humo.
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha muda huu juu ya kifo hicho na kwamba bado haijafahamika chanzo cha kifo chake.
Kwa sasa mwili wa marehmu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya rufaa ya KCMC .
Ndugu wakiwemo watoto wa marehemu wamefika Hospitalini hapo na kuomba mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi kutokana na kifo kuwa ni cha ghafla.
Lema alisema, Mzee Ndesamburo alifika ofisini kwake majira ya asubuhi na alionekana mwenye afya njema, ilipofika majira ya saa nne hali ilibadilika na kushindwa kuendelea na majukumu yake.
Ndipo walipomkimbiza KCMC kwa ajili ya matibabu na alifariki dunia akiwa kitengo cha emergency, Taarifa zaidi tutajulishana kadri zitakapokuwa zikitufikia.
No comments:
Post a Comment