Teknolojia : Uchumi wa Kidijiti ni Kipaumbele kwa Zanzibar - Rais Dkt. Mwinyi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

Monday, 26 January 2026

Teknolojia : Uchumi wa Kidijiti ni Kipaumbele kwa Zanzibar - Rais Dkt. Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka kipaumbele kikubwa katika uendeshaji wa uchumi, utoaji wa huduma za Taasisi za Umma pamoja na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya kidigitali.


Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 26 Januari 2026 alipokutana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki, pamoja na watendaji wakuu wa Wizara hiyo, Ikulu Zanzibar.

Amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara za Muungano na Zanzibar, ikiwemo kuharakisha ujenzi wa Kituo cha Ukusanyaji wa Taarifa (Data Centre) Zanzibar, kuboresha miundombinu ya mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa intaneti ya kasi.

Kwa upande wake, Waziri Angellah Kairuki amemhakikishia Rais Dkt. Mwinyi kuwa Wizara yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na Zanzibar ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano zilizo salama, za uhakika na zenye viwango vya kitaifa na kimataifa.






No comments:

Post a Comment