Na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam.
Novemba
5, mwaka huu ni mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alioapishwa kuwa kiongozi na Amri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi hii.
Katika
kipindi cha mwaka mmoja cha utawala wa Rais Magufuli nchini, Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa upande wake umesaidia
Watanzania wanaopata huduma za Jamii kupitia PSPF kuongezeka kutoka
394,494 hadi kufikia 444,679 ikiwa ni sehemu ya utekeleza wa agizo
lake.
Hatua
hii ya PSPF imelenga kutekeza agizo na kutimiza ahadi ya Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyokuwa akitoa ya kuhakikisha kuwa
Watanzania wengi wanufaika na huduma za Hifadhi za Jamii ikiwemo huduma
za Bima za afya wakati wa kampeni na baada ya kuingia madarakani.
Kwa
mujibu wa taarifa ya mwaka mmoja kwa upande wa Mfuko wa PSPF iliyotolewa
na Costantina Martin kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF ,idadi hiyo
hii inajumuisha Watanzania walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi
nchini.
Kundi
hili kubwa lilikuwa limesaulika kujumuishwa katika hifadhi ya jamii ,
lakini baada ya Mhe. Rais Magufuli kulizungumzia katika kampeni zake
hivi sasa mwamko wa kujiunga na hifadhi ya jamii umeongezeka na PSPF
imeanza kulitekeleza agizo hilo kwa kuwahamasisha wananchi waliopo
katika sekta isiyo rasmi na sekta rasmi kuchangia na kujiunga katika
Bima ya Afya.
Katika
kuhakikisha kuwa azma hiyo inatimizwa tayari PSPF imeingia makubaliano
na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa lengo la kufikisha huduma za
afya kwa watanzania wengi ambao wapo katika sekta isyo rasmi na hivyo
kujenga jamii yenye afya bora inayochangia katika ujenzi wa nchi.
Chini
ya makubaliano yanawasaidia wanachama wa PSPF walio katika Mpango wa
Uchangiaji wa Hiari kuweza kupata ya tiba kupitia NHIF kwa gharama ya
shilingi 76,800/- kwa mwaka katika hospitali mbalimbali ziliingia
makubaliano na Mfuko huo wa Bima ya Afya.Mpango huo wa PSPF unaounga
mkono juhudi za Rais Magufuli za kutaka kuhakikisha kuwa wananchi wengi
wanapata huduma na matibabu nchi nzima kwenye vituo vyote
vilivyosajiliwa na NHIF kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa kwa
gharama nafuu.
Hivi
sasa huduma hiyo ya PSPF kuwadhamini wananchama wake kwa ajili ya kupata
matibabu imesaidia watanzania wengi sana kunufaika na huduma hii
husasan katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli.Akifungua rasmi
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Rais Magufuli alisema
kuwa dhamira ya kujenga uchumi wa kisasa na suala la kupambana na
umaskini linakwenda sambamba na kuwa na wananchi wenye afya bora.
Aliongeza
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha wananchi wanapata huduma
bora za afya kwa kuhamasisha wananchi wengi wanajiunga na Bima ya
Afya.Katika kutekeleza hilo PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya(NHIF) imeshawafikia Watanzania 2,710 walio katika sekta
isiyo rasmi kuanza kunufaika na huduma za Afya kupitia PSPF.Mbali na
sekta ya afya , katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli PSPF kwa
upande wake imesaidia kuhakikisha kuwa Tanznaia inakuwa Nchi ya Viwanda
kwa lengo la kutoa ajira kwa Watanzania walio wengi.
Viwanda hivyo ambavyo PSPF imewekeza ni pamoja na 21st Century cha Morogoro, Saruji Tanga.Martin
ameongeza kuwa hivi sasa PSPF imejipanga kuwekeza katika Kituo cha
Biashara cha Kurasini (Kurasini Logistic Center) kwa lengo la kuchochea
uwekezaji wa viwanda na kutoa ajira kwa wananchi.
Viwanda
vingine ambavyo PSPF imejipanga kuwekeza ni kile cha Nguo cha Urafiki,
Morogoro Canvas Mill na Kiwanda cha Viatu Karanga kilichopo Moshi.Hatua
hiyo iliyoanza kutekelezwa na PSPF ni sehemu utekelezaji hotuba ya Mhe.
Rais Magufuli wakati anafungua rasmi Bunge 11 mjini Dodoma mwishoni mwa
mwaka jana ambapo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaweka mkazo
katika ujenzi wa viwanda ili mwaka 2020 idadi ya ajira itokanayo na
viwanda ifikie asilimia 40 ya ajira zote hapa nchini.
PSPF
ilianzishwa kwa sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Watumishi wa
Umma namba 2 ya mwaka 199 . sura ya 371 na inatoa huduma za Hifadhi ya
Jamii katika Mapngo wa lazimana wa hiyari.
No comments:
Post a Comment