Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Muwada
wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 umesomwa mara ya pili
Bungeni mjini Dodoma ukiwa na lengo la kuifanya tasnia ya habari nchini
kuwa taaluma kamili.
Wiziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema hay oleo
Bungeni Dodoma alipokuwa akiwasilisha Muswada huo, huku akisisitiza kuwa
una sehemu kuu nane ambazo zinaufanya kuleta mageuzi katika tasnia ya
habari nchini na kuifanya kuwa taaluma kamili itayowaletea heshima
wanahabari na tasnia hiyo kwa ujumla.
“Hatuwezi kwa na vyombo vya habari makini kama hatutakuwa na wanahabari wenye taaluma ya habari nchini” alisema Nape.
Katika
kuonesha ushirikishwaji wa wadau katika kutoa maoni yaliyolenga
kuboresha Muswada huo, Waziri Nape amesema kuwa kumekuwa na
ushirikishwaji mkubwa wenye wigo mpana kutoka kwa mwananchi mmoja mmoja,
wanataaluma wa habari, wanasheria kupitia Chama cha Mawakili Tanzania
(TLS), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Wamiliki wa vyombo vya
habari (MOAT) na Taasisi ya Wanahabari Kusini mwa Afrika, tawi la
Tanzania (MISA-TAN).
Wadau
wengine walitoa maoni yao ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC), Sikika, Wabunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii pamoja na michango ya Wabunge kupitia Kamati nyingine
ambao umesaidia katika kuboresha Muswada huo wenye dhamira ya kuleta
ufanisi katika sekta ya habari.
Miongoni
mwa maeneo ambayo wadau hao wameyafanyia maboresho ili Muswada uwe na
tija ni pamoja na kuainisha haki na wajibu wa wananhabari ikiwemo uhuru
wa kukusanya, kuhariri na kuchapisha au kutangaza habari pamoja na
kuainisha haki ya chombo cha habari kukata rufaa kwa kuzingatia mfumo wa
wazi na wa kidemokrasia kupitia vyombo vya kutoa haki ikiwemo mahakama
huku Jaji Mkuu akiweka utaratibu wa kusikilizwa haraka kwa kesi za
masuala ya kihabari.
Maboresho
mengine yaliyofanya ni uwakilishi wa wanahabari katika Bodi ya Ithibati
kwa kuzingatia uwiano wa wajumbe kutoka sekta ya habari ya umma na ya
binafsi, kuviondolea adhabu vyombo vya habari au wamiliki baadhi ya
makosa ya mwandishi ambapo atawajibishwa na Bodi ya Ithibati akiwa yeye
ni mwanataaluma kamili kukutenda makosa ya kimaadili na vyombo vya dola
kukamata mitambo na vifaa vya wanahabari maboresho yanaonesha kazi hiyo
sasa itafanywa na Jeshi la Polisi kwa sheria ya Mwenendo wa Mkosa ya
Jinai badala ya kazi hiyo kufanywa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari.
Zaidi
ya maboresho hayo, Waziri Nape ameongeza kuwa maboresho mengine ni
kuhusu mitambo kutohusika moja kwa moja kwa kosa la gazeti ambalo
limechapisha habari yenye makosa ya kisheria dhidi ya watu au taasisi
mbalimbali.
Waziri
Nape amefafanua kuwa chimbuko, muktadha na mchakato wa kuandaa Muswada
huo unatokana na baadhi ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1984 ambapo haki ya
kikatiba ya kutafuta, kupokea na kutoa habari imeainishwa kwenye Ibara
ya 18 (b) pamoja na mikataba mbalimbali ya kimataifa ya inayoainisha
haki na wajibu wa sekta ya habari.
Mkatabahiyo
ya Kimataifa ni ule wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966 ambao
Tanzania iliuridhia Juni 11, 1984 pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki za
Binadamu na Watu 1981 ambao nao uliridhiwa Februari 18, 1984.
Akinukuu
maneno mbalimbali ya watu maarufu duniani juu ya masuala ya habari
akiwemo Rais wa Marekani Thomas Jefferson Januari 16, 1789, Rais wa
zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Muasisi wa Taifa la India
Mahatma Ghandhi, Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill (1806-1873)
pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Nape akinukuu
maneno ya mmoja wa viongozi hao Mahatma Ghandhi aliamini kuwa uhuru wa
kweli wa kujieleza ni ule unaoweka mbele heshima ya watu wengine na
kuwalinda dhidi ya dhara, kebehi, kejeli na madhara mengine huku Baba wa
Uhuru wa Habari John Stuart Mill akibainisha dhima ya uhuru wa vyombo
vya habari na umuhimu wa kuwa huriu unapaswa kuzingatia ukomo wa haki ya
kupata habari kuwa unakoma pale haki za watu wengine zinapoanzia.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba amesema kuwa kamati yake imeufanyia
kazi Muswada huo kupitia maoni ya wadau na watu mbalimbali nchini ambayo
ndio yamakuwa msingi wa kuuboresha muswada huo.
Serukamba
aliongeza kuwa kati ya miswada ambayo wananchi wengi wameisoma na
kusikilizwa ni Muswada habari ambao umejadiliwa kwa njia mbalimbali
ikiwemo vyombo vya habari; kwenye magazeti, kwenye radio na Televisheni
kupitia vipindi maalum vya kujadili Muswada huu na maoni yao mengi
yameingizwa kwenye Muswada huu” alisema Serukamba.
No comments:
Post a Comment