Matukio : Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Moi wafanya upasuaji wa vichwa maji na mgongo wazi mnazi mmoja Zanzibar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 4 November 2016

Matukio : Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Moi wafanya upasuaji wa vichwa maji na mgongo wazi mnazi mmoja Zanzibar

Daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya MOI Othman Kiloloma akimueleza Waziri wa Afya Zanzibar (hayupo pichani) jinsi Taasisi hiyo inavyookoa maisha ya watoto wanaokabiliwa na maradhi hayo, (kulia) ni Afisa Habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na ujumbe wa Taasisi ya MOI na GSM Foundation ambao wapo Zanzibar kuwafanyia upasuaji watoto wenye vichwa vikubwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Dkt. Mohammed Ali Haji wa Kitengo cha upasuaji vichwa maji na mgongo wazi wa Hospitali ya Mnazimmoja akizungumzia ukubwa wa tatizo hilo katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Dkt. Yassin Juma kutoka Kitengo cha MOI akiwa katika maandalizi ya kumfanyia upasuaji wa kichwa mmoja ya watoto waliofika Hospitali ya Mnazi mmoja kufanyiwa tiba hiyo.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo wa nne (kulia) akiwa na Dkt. Othman Kiloloma watatu (kulia)wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara na maafisa wa GSM Foundation. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment