Mtaalamu
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akitoa
semina juu ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs)
katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo mkoani Arusha.(Picha na
Ferdinand Shayo).
Maafisa
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wamefanya ziara ya kutembelea
Chuo cha Tumaini tawi la Arusha ikiwa ni pamoja na kutoa semina juu ya
Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ikiwemo kufuta
umasikini, kuondoa njaa na kuhakikisha upatikanaji wa maji.
Mtaalam
wa Programu kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini, Amon Manyama amesema kuwa wasomi na wanafunzi walioko vyuoni
wanapaswa kuelewa vizuri malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ya Umoja
wa Mataifa ili waweze kuyatimiza katika ngazi zao hasa ukizingatia kuwa
wanachuo ni wataalamu watarajiwa,na viongozi wa kesho.
Manyama
amesema kuwa taasisi,mashirika na jamii pamoja na serikali ina jukumu
kubwa la kutekeleza malengo hayo ili kuondoa umasikini, kujenga uchumi
endelevu,kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mtaalam
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu amesema kuwa
vijana hususan wanavyuoni wanapaswa kuwa mambalozi wazuri wa
kuyatangaza malengo ya maendeleo endelevu ya UN ili yaweze kutimia na
dunia iwe ni sehemu bora zaidi ya kuishi kwa kila mtu.
Temu
amesema kuwa UN ina mpango wa kuwafikia vijana walioko vyuoni na mitaani
ili waweze kuelewa vizuri juu ya malengo 17 ya maendeleo endelevu ya
Umoja wa Mataifa na kujua jukumu walilonalo ndani ya malengo hayo.
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog, Arusha

No comments:
Post a Comment