Maisha na Usafi : Wafanyakazi Hospitali ya Muhimbili wafanya usafi kutekeleza agizo la Rais. - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Jun 2016

Maisha na Usafi : Wafanyakazi Hospitali ya Muhimbili wafanya usafi kutekeleza agizo la Rais.


Ikiwa Jumamosi hii ya Juni 25, ni ya mwisho wa mwezi wafanyakazi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili watekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, John Pombe Magufuli kwa kufanya usafi katika sehemu mbalimbali za hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakifanya usafi LEO ikiwa ni kutekeleza agizo la rais la kufanya usafi kila mwishoni mwa mwezi. 

 Kutoka kulia Chindemba Lingwana, Patrick Rogath ambaye ni Mkuu Idara ya Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwenye hospitali hiyo, Christian Mtei na Fred Felix wakifanya usafi katika jengo la utawala LEO. Shughuli za usafi zikiendelea LEO katika Hospitali hiyo.
 HAPA KAZI TU.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Post Top Ad