Wabunge wakiondoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Naibu Spika kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge leo.
Wabunge
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge
kufuatia Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe. Tulia Ackson kutangaza
kuliahirisha Bunge leo mjini Dodoma.Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson
Mwansasu akiongoza kikao cha 32 cha Mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 32 cha Bunge hilo mjini Dodoma
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla akijibu maswali ya wabunge kuhusu sekta ya Afya Bungeni
mjini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mhe. Mwita Mwikwabwe akisoma kitabu cha Kanuni za Kudumu za Bunge ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Mbunge
wa Nzega Mhe. Hussein Bashe (CCM) akizungumza jambo na Mbunge wa
Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kulia) nje ya ukumbi wa
Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha 32 cha mkutano wa tatu wa
Bunge leo mjini Dodoma.
Wanafunzi
wa shule ya Sekondari Barbro Johansson iliyoko jijini Dar es salaam
wakiondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya
kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwenye
wizara yake Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo na Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba nje ukumbi wa Bunge.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akizungumza jambo na wabunge leo mjini Dodoma.
Mbunge
wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto)
akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia
ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mbunge wa Kigoma Mhe. Peter Selukamba akijadiliana jambo na Mbunge wa Nzega mjini Mhe. Hussein Bashe (kushoto)Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu nje ya Ukumbi wa Bunge mjini.
Kikao cha 32 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asubuhi.
Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akimweleza jambo Mwenyekiti
wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi
nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum -
DODOMA
No comments:
Post a Comment