Waandishi wa Habari 'Bloggers' kutoka Tanzania Bloggers Network (TBN) ambao wameshiriki kikamilifu kwenye Kamati ya maandalizi ya mkutano huo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Waziri Wizara ya Habari Michezo Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi ametoa pongezi kwa Waandishi wa Habari kwa juhudi zao za kuhabarisha umma kuhusu taarifa mbalimbali za serikali, ikiwa ni pamoja na Mkutano Mkuu wa Nishati uliohudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali, uliofanyika Jijini Dar es Salaam mwezi uliopitamwaka huu.
Prof.Kabudi amesema hayo Februari 13 alipokua mgeni rasmi kwenye mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini uliofanyika kwenye Ukumbi wa New Generation, Kisasa Dodoma nankuhudhuriwq na wanahabari wakongwe bloggers kutoka Tanzania Bloggers Network (TBN) na wanamitandao mbalimbali.
Prof.Kabudi amewasihi wanahabari kuwa ni wajibu wao waendelee kuelimisha wananchi kuhusu jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa hiyo ni ajenda ya kitaifa.
Meza kuu.
Baadhi ya waandishi wa habari wameelezea kuridhishwa na hatua ambazo serikali imekuwa ikichukua katika kuimarisha sekta ya habari.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Greyson Msigwa, amewashauri waandishi wa habari kuwa, kupitia Mkutano huu, wanapaswa kuzingatia weledi katika taaluma yao hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kulinda usalama wa taifa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Saida Muki, amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuwa makini na matumizi ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI) wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ili wasiwasilishe maudhui yanayoweza kupotosha umma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewakaribisha Waandishi wa Habari Jijini Dodoma na kuwata watembelee maeneo mbalimbali ambayo yamejengwa majengo ya kisasa na kusema kuwa Dodoma inaendelea kukua kiuchumi na kuleta chachu ya maendeleo kila uchao. ![](https://lh3.googleusercontent.com/-RohDZ3MyLUU/Z65VL3plCiI/AAAAAAAAlyU/_h4A0HNm1LYsTPbt4XspP3ji_J0dIBu0QCNcBGAsYHQ/s1600/IMG_ORG_1739477900184.jpeg)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari, amesema mkutano huu umeandaliwa ili kujadili masuala muhimu yanayohusu sekta ya habari na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokikabili sekta hiyo.
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, Dkt. Bakari amewasihi waandishi wa habari kutumia taaluma zao vizuri, kuhabarisha umma kuhusu hatua zote za uchaguzi hadi siku ya kupiga kura.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Wajibu wa vyombo vya utangazaji kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025" amesema Dkt. Jabir
No comments:
Post a Comment