Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Mwanza, Geofrey Makondo, akizungumza na baadhi ya wateja wao wa Mkoani Mwanza, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa maboresho ya huduma ya Stanbic Private Banking, mkoani humo jana. Private Banking ni huduma binafsi za kifedha kwa wateja wenye ukwasi mkubwa, wakiwemo wamiliki wa biashara, wawekezaji, wataalamu wa sekta mbalimbali, na viongozi wa biashara na inawawezesha kusimamia na kukuza amana zao kwa ufanisi zaidi kupitia ushauri wa kifedha, uwekezaji, na mipango ya urithi wa mali.
Na mwandishi wetu Mwanza.
Mkuu wa kitengo cha Private Banking wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shangwe Kisanji (wa nne kushoto), akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wa Tawi la Mwanza, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa maboresho ya huduma ya Stanbic Private Banking, mkoani humo jana. Private Banking ni huduma binafsi za kifedha kwa wateja wenye ukwasi mkubwa, wakiwemo wamiliki wa biashara, wawekezaji, wataalamu wa sekta mbalimbali, na viongozi wa biashara na inawawezesha kusimamia na kukuza amana zao kwa ufanisi zaidi kupitia ushauri wa kifedha, uwekezaji, na mipango ya urithi wa mali.

Uzinduzi huu ni hatua muhimu ya kimkakati wa upanuzi wa benki, ukihakikisha kuwa wateja wa Mwanza ikiwa ni jiji la pili kwa ukubwa Tanzania na kituo kikubwa cha biashara, wanapata huduma binafsi za kibenki, ushauri wa uwekezaji, na mipango ya usimamizi wa mali inayoendana na mahitaji yao ya kifedha.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Shangwe Kisanji, Mkuu wa kitengo cha Private Banking wa Benki ya Stanbic Tanzania, alieleza umuhimu wa kutoa suluhisho za kifedha zilizo maalum kwa wateja walengwa, zinazolenga kusaidia wateja wa Mwanza kufanikisha malengo yao ya kifedha.
“Huduma hii ya Private Banking si tu ni suala la usimamizi wa fedha, ni ushirikiano kati yetu na wateja wetu katika kujenga, kukuza, na kulinda mafanikio yao kwa vizazi vijavyo. Tunatambua kuwa wateja wetu wa Mwanza wanahitaji suluhisho maalum za kifedha, na ndiyo maana huduma ya Private Banking yetu imezinduliwa mahsusi kwa ajili yao. Kuanzia mipango na ushauri wa uwekezaji hadi mikopo maalum, na usimamizi wa mali za familia, benki ya Stanbic inatoa utaalamu na nyenzo zinazohitajika kufanikisha malengo ya kifedha ya wateja wetu.”
“Wateja wanaojiunga na huduma ya Private Banking ya Benki ya Stanbic watapata fursa ya kunufaika na huduma za kifedha za kipekee, ambazo zinakwenda mbali zaidi ya huduma za kibenki za kawaida kama vile ushauri wa wa mwongozo wa kitaalamu wa jinsi ya kujenga, kukuza, na kulinda amana zao, hii ikijumuisha mkakati wa uwekezaji, usimamizi wa hatari wa kifedha, na ushauri wa utofauti wa uwekezaji ili kuwasaidia wateja wenye ukwasi mkubwa kuongeza thamani ya mali zao”, alisema Bi. Shangwe.
Alisema kwa upande wa Huduma za benki zinazowezesha mahitaji ya kibiashara na binafsi, ikiwemo ununuzi wa mali, upanuzi wa biashara, na uwekezaji katika miradi mikubwa, wateja wa Private Banking watapata mikopo maalum yenye masharti nafuu na viwango bora vya riba.
Aidha aliongeza kuwa wateja wa Private Banking watakuwa na msimamizi binafsi wa akaunti zao anayewapa huduma za kifedha zilizo maalum kwa mahitaji yao na kuhakikisha miamala yao inafanyika kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.
“Kupitia mtandao wa Stanbic na Standard Bank Group, wateja watapata huduma za kifedha za kimataifa, ikiwa ni pamoja na ushauri wa uwekezaji wa nje ya nchi, miamala ya nchi jirani, na usimamizi wa amana katika masoko ya kimataifa, hivyo kuhakikisha kuwa amana zao zinaendelea kukua popote walipo.
“Benki pia itatoa ushauri kwa wateja wake na familia zao kwa kutoa mpango wa elimu ya kifedha na mipango ya urithi wa mali. Mpango huu unalenga kuwaelimisha vizazi vijavyo juu ya usimamizi wa fedha, mikakati ya uwekezaji, na maamuzi sahihi ya kifedha, kuhakikisha kuwa amana zao zinadumu kwa miaka mingi ijayo”, aliongeza Bi. Shangwe.
Naye mmoja wa wateja aliyehudhuria katika hafla hiyo, Bi. Fatma Kimwaga aliipongeza benki ya Stanbic kwa jinsi inavyowajali wateja wake, hususani katika eneo la ushauri wa masuala yanayohusu uwekezaji, elimu ya kifedha pamoja usimamizi wa mali za familia kwa ni maeneo yanayohitaji kupewa kipaumbele kwa mustakabali wa ustawi wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, familia na jamii.
“Naipongeza sana Stanbic Bank kwani kwa kupitia Stanbic Private Banking nina imani hata kama nikiwa sipo duniani watoto wangu wataelewa nini cha kufanya, kuna wafanyabiashara wengi wanakufa bila kuacha mpango wa uhakika kwa watoto wao hivyo kujikuta familia ikiangukia katika migogoro ya muda mrefu”, alisema Bi. Fatma.
Uzinduzi wa wa huduma ya Private Banking ya Benki ya Stanbic jijini Mwanza ni moja wapo wa mikakati ya kupanua wigo wa huduma katika majiji mengine kama Mbeya, Arusha, Dodoma, na maeneo mengine

Mkuu wa kitengo cha Private Banking wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shangwe Kisanji (kushoto), Meneja wa Benki ya Stanbic, Tawi la Mwanza, Geofrey Makondo (katikati), pamoja na mteja wa benki hiyo, Meneja wa Kampuni ya GardaWorld, Tawi la Mwanza, Levina Beal, wakizindua rasmi maboresho ya huduma ya Stanbic Private Banking, mkoani humo jana. Private Banking ni huduma binafsi za kifedha kwa wateja wenye ukwasi mkubwa, wakiwemo wamiliki wa biashara, wawekezaji, wataalamu wa sekta mbalimbali, na viongozi wa biashara na inawawezesha kusimamia na kukuza amana zao kwa ufanisi zaidi kupitia ushauri wa kifedha, uwekezaji, na mipango ya urithi wa mali.

Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Mwanza, Geofrey Makondo (kulia), mmoja wa wateja wa benki hiyo mkoani Mwanza, Hussein Murtaza (katikati), na Mkuu wa kitengo cha Private Banking wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shangwe Kisanji, wakizindua rasmi maboresho ya huduma ya Stanbic Private Banking, mkoani humo jana. Private Banking ni huduma binafsi za kifedha kwa wateja wenye ukwasi mkubwa, wakiwemo wamiliki wa biashara, wawekezaji, wataalamu wa sekta mbalimbali, na viongozi wa biashara na inawawezesha kusimamia na kukuza amana zao kwa ufanisi zaidi kupitia ushauri wa kifedha, uwekezaji, na mipango ya urithi wa mali.
Mkuu wa kitengo cha Private Banking wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shangwe Kisanji (kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wao wa Mkoani Mwanza, mara baada ya uzinduzi rasmi wa maboresho ya huduma ya Stanbic Private Banking, mkoani humo jana. Private Banking ni huduma binafsi za kifedha kwa wateja wenye ukwasi mkubwa, wakiwemo wamiliki wa biashara, wawekezaji, wataalamu wa sekta mbalimbali, na viongozi wa biashara na inawawezesha kusimamia na kukuza amana zao kwa ufanisi zaidi kupitia ushauri wa kifedha, uwekezaji, na mipango ya urithi wa mali. Katikati ni Levina Beal na Fatma Kimwaga.
Mkuu wa kitengo cha Private Banking wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shangwe Kisanji, akizungumza na baadhi ya wateja wao wa Mkoa wa Mwanza, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa maboresho ya huduma ya Stanbic Private Banking, mkoani humo jana. Private Banking ni huduma binafsi za kifedha kwa wateja wenye ukwasi mkubwa, wakiwemo wamiliki wa biashara, wawekezaji, wataalamu wa sekta mbalimbali, na viongozi wa biashara na inawawezesha kusimamia na kukuza amana zao kwa ufanisi zaidi kupitia ushauri wa kifedha, uwekezaji, na mipango ya urithi wa mali.
No comments:
Post a Comment