Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Bw. Florenso Kirambata (kulia) akiwa na baadhi ya wageni waliofika kwenye banda la Tanzania wakati wa Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama ITB-Berlin yanayoendela huko nchini Ujerumani.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Bw. Florenso Kirambata (kulia) akiwa na baadhi ya wageni waliofika kwenye banda la Tanzania wakati wa Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama ITB-Berlin yanayoendela huko nchini Ujerumani.Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Bw. Florenso Kirambata (katikati) wakati wa Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama ITB-Berlin yanayofanyika yanayoendelea nchini Ujerumani kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bodak Adventure Safari Bi.Davina Rukaka na Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya OverCross Bw. Maik Schneider kutoka Ujerumani.
Na. Mwandishi wetu
Tanzania imeendelea kuimarisha nafasi yake katika ramani ya utalii duniani kwa kushiriki kikamilifu kwenye maonyesho makubwa ya utalii ya ITB-Berlin 2025, yaliyofanyika nchini Ujerumani kuanzia Machi 4,2025 hadi Machi 6.
Ushiriki huu umetoa fursa muhimu kwa wadau wa utalii wa Tanzania kuonesha vivutio vilivyopo nchini na uwezo wa huduma ya ukarimu iliyopo nchini.
Miongoni mwa washiriki waliovutia sana kwenye maonyesho hayo ni Turaco Collection, ambao wana hoteli za kifahari katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Florenso Kirambata, aliongoza timu yake kuonyesha bidhaa na huduma za hoteli zao, zikiwemo Element By Westin Marriott na Delta By Marriott (Dar es Salaam), Turaco Ngorongoro Valley Lodge, Turaco Manyara View Lodge, Turaco Nungwi Beach Resort, Turaco Spice Tree Stone Town, na Beyt Aly Salaam-By Turaco (Zanzibar).
Kirambata alisema kuwa maonyesho hayo ni jukwaa muhimu la kujitangaza, kubadilishana uzoefu, na kuelewa mahitaji ya wateja wanaobadilika. Alisisitiza kuwa Turaco Collection imejitolea kutoa huduma bora na uzoefu wa kipekee kwa watalii wanaotembelea Tanzania.
"Ushiriki wa Tanzania kwenye ITB-Berlin 2025 una manufaa mengi.Tupo hapa kuitangaza Tanzania Kimataifa, kuwaonesha nini tunaweza kuwapa katika sekta na watalii kutoka kote ulimwenguni.
Tunapata pia fursa ya kujenga uhusiano na wadau wa utalii kutoka nchi nyingine, na kubadilishana uzoefu na maarifa" alisema Kirambata.
Tanzania inaendelea kuweka juhudi kubwa katika kukuza sekta ya utalii, na ushiriki wake kwenye maonyesho ya ITB-Berlin 2025 ni moja ya hatua muhimu katika kufikia malengo hayo. Serikali na wadau wa utalii wanafanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kivutio kikuu cha utalii barani Afrika.
No comments:
Post a Comment