Mabalozi
wa Chakula na Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Shirika la Oxfam kwa
upande wa Tanzania Shamim Mwasha ambaye pia ni Fashion Blogger(wa kwanza
kushoto), Jacob Stephen 'JB' Msanii Maarufu wa Bongo Movie(wa katikati)
na Khadija Mwanamboka wakitangaza majina 19 ya washiriki wa shindano la
Mama shujaa wa chakula 2016 msimu wa tano.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster(aliyesimama)
akiwapongeza washiriki wote waliojaza fomu za kushiriki shindano la
mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016 kutoka mikoa mbalimbali
nchini.
Meneja
utetezi kutoka Oxfam Tanzania Eluka Kibona akitoa maelezo kuhusu
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kuwa linaendeshwa Tanzania,Nigeria na
Ethiopia ambapo alisema lengo la shindano ni kutambua mchango wa
wanawake katika mapambano dhidi ya umasikini na kuleta uhakika wa
chakula.
Afisa
uhakiki wa ubora kutoka TBS Stela Mroso akisisitiza jambo kuhusu
ushirikiano wao kama Shirika la Viwango la TBS na Oxfam Tanzania
kuhakikisha wanatetea wanawake.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Kilimo Paskarina Kayuma akitoa Shukurani kwa Shirika
la Oxfam Tanzania kwa kuendelea kuwanyanyua wanawake katika kilimo na
amewaomba juhudi hizo ziendelee.
Miongoni
mwa majaji Edna Kiogwe mshiriki wa mama Shujaa wa Chakula msimu
uliopita(Kulia) pamoja na Fredy Njeje kutoka Blogs za Mikoa (Kushoto)
wakielezea namna usaili ulivyofanyika mpaka kuwapata washiriki 19 katika
shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano kwa mwaka 2016.
Aliyekuwa
mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita Ester
Kulwa akionesha kanda zote ambazo washiriki wametokea.
Baadhi
ya wageni wakiwa katika Hafla fupi ya kutangaza majina 19 ya washiriki
katika shindano la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016.
Mshindi
wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 linaloendeshwa na Shirika la
Kimataifa la Oxfam Tanzania kutoka Morogoro Caroline Chelele
akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Aliyekuwa
Mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pili Kashinje
akizungumza jambo wakati wa Hafla fupi ya kutangaza washiriki shindano
la Mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016.
Suhaila Thawer ambaye ni 'Public Forum Officer' kutoka Shirika la Oxfam Tanzania akitoa neno la Shukurani.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa pili kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na Majaji,Wafanyakazi wa Oxfam pamoja na Mabalozi
wa Chakula na Kampeni ya Grow.
Waliosaidia
katika kupitia Fomu za Mama shujaa wa Chakula kwa hatua ya Mwanzo
kutoka Taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa saba kutoka kulia).
Hatimaye
19 watajwa kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa
tano kwa mwaka huu 2016, ambapo fomu 3000 zilizotumwa na wakulima
wanawake kote nchini, fomu 1795 zilipitiwa na kuwapata washiriki hao
ambao wataanza kutembelewa mmoja mmoja ili kuhakiki iwapo kile
walichokijaza kwenye fomu kinaoana na hali halisi. Mashindano ya Mama
Shujaa wa Chakula 2016, linatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Enguiki
kilichopo Monduli mkoani Arusha, kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 16 na
kurushwa katika Runinga ya ITV.
Akizungumza
wakati wa kutangaza majina hayo, mmoja wa majaji wa shindano hilo Jacob
Stephen ‘JB’ ambaye ni muigizaji maarufu wa Filamu Tanzania alisema
katika uchambuzi wa fomu hizo walikuwa ni wanawake wakulima ambao
wanaelimu ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wale wadogo
wadogo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster alisema shindano hilo limeanza
kuendeshwa kuanzia mwaka 2011 na sasa ni msimu wa tano na limefanikiwa
kuwaunganisha wanawake wakulima wadogo wadogo ambao ni asilimia 70 ya
wanawake nchini. Alisema majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na
kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao
ili changamoto zilizopo zitatuliwe.
Alisema
majaji wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki
ambao watakuwa mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto
zilizopo zitatuliwe. Aliongeza kuwa shindano la mama shujaa wa Chakula
linaendeshwa katika nchi tatu Afrika ikiwemo Nigeria, Ethiopia na
Tanzania. Ambapo Tanzania wamepita katika mikoa mbalimbali na kukusanya
wanawake wakulima wadogo wadogo ambao tunaamini kwa kuwa pamoja wanaweza
kupaza sauti kwa watunga sera kuhusu changamoto wanazokutana nazo.
Afisa
Uhakiki wa Ubora TBS, Stela Mroso alisema shirika la viwango nchini
liliungana na Oxfam mwaka jana ili kuhakikisha wanawaleta wanawake
pamoja na kutoa elimu zaidi kuhusu kilimo chenye ubora na mazao
yanayoweza kuwa na viwango vya kimataifa. Alisema bila viwango wanawake
hawawezi kufanya biashara, huku akitoa wito kwao kujitokeza ili
kuangalia ubora wa mazao wanayozalisha. Aliongeza kuwa asilimia 80 ya
wanawake nchini wanajishughulisha na Kilimo kwa hiyo ni muhimu chakula
kinachozalishwa kiwe katika ubora na afya pia kiweze kuzaliswa
Kimataifa.
Washiriki
wa Mama Shujaa wa Chakula 2016 kuwa ni Betty Nyange (62) Mkoa wa
Morogoro, Monica Charles Mduwile (44) Mkoa wa Dodoma, Neema Gilbet
Uhagile (29) Mkoa wa Njombe, Mary Christopher Lyatuu (29) Mkoa wa
Arusha, Loyce Daudi Mazengo (39) Mkoa wa Singida, Anjela Chogsasi
Mswete (48) Mkoa wa Iringa, Lucina Sylivester Assey (54) Mkoa wa
Shinyanga, Marta Massesa Nyalama (50) Mkoa wa Kaskazini Unguja,
Christina Machumu (42) Mkoa wa Mara, Happiness Paulo Raulent (35) Mkoa
wa Kagera. Mary Bony Soko (42) Mkoa wa Ruvuma, Mary Ramadhani Mwiru (39)
Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanaid Alli Abdalla (53) Mkoa wa Mjini
Magharibi, Maria Alfred Mbuya (43) Mkoa wa Mbeya, Eliza Richard Mwansasu
(30) Mkoa wa Rukwa, Mwajibu Hasani Binamu (46) Mkoa wa Mtwara, Eva
Haprisoni Sikaponda (40) Mkoa wa Songwe, Hidaya Said Musa (40) Mkoa wa
Tanga na Mwasiti Salim Mazuri (40) Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya
Kinondoni.
No comments:
Post a Comment