Matukio :Spika Mstaafu Anna Makinda atembelea banda la Benki ya DCB katika maonyesho ya nane nane Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 8 August 2017

Matukio :Spika Mstaafu Anna Makinda atembelea banda la Benki ya DCB katika maonyesho ya nane nane Dodoma


Spika Mstaafu Anna Makinda ameipongeza DCB Commercial Bank kwa huduma bora za kibenki inayotoa hasa huduma za mikopo kwa wajasirimali wadogo wadogo na kuwakwamua katika hali ya umasikini.


Makinda amewaasa DCB Commercial Bank kujikita zaidi kutoa huduma hii kwa wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambao ndiyo wengi nchini ili kuboresha hali za maisha yao kwa kuwapatia mikopo.


Hayo aliyasema wakati alipotembelea banda la DCB Commercial bank katika maonesho ya nane nane kanda ya kati yanayoendelea mkoani Dodoma. Makinda aliongezea kuwa ili kuwezesha wajasiriamali wengi DCB Benki haina budi kupeleka huduma hii ya mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambako kuna uhitaji mkubwa wa huduma hii ya mikopo ya vikundi Sambamba na utoaji wa mikopo hii ya vikundi kwa wajasiriamali wadogo wadogo.


Makinda ameasa DCB kuwaunganisha wajasiriamali hawa na huduma ya bima ya afya kutoka NHIF na pia bima ya taifa ya Jamii ili wateja hawa au familia zao wanapougua wapate msaada wa matibabu kwa unafuu hivyo kuwafanya wawe na afya na kuweza kurejesha mikopo .


Alisisituza kuwa mteja akiugua ile pesa ya marejesho ataitumia katika kugharamia matibabu hivyo kuitia hasara benki, kumbe akijiunga na mifuko ya afya ya jamii atapata matibabu bure hivyo benki haitaathirika. Alisema makinda.


Akimkaribisha kwenye banda na kuelezea huduma zinazotolewa na DCB Commecral Bank, Meneja masoko wa DCB benki Boyd Mwaisame alitaja huduma za DCB zinazopatikana katika banda la benki hiyo viwanja vya maonesho nane nane Mzuguni Dodoma kuwa ni pamoja na kufungua akaunti za kuweka akiba kwa watu binafsi, akaunti za wanafunzi, akaunti za muda maalumu, akaunti za biashara na huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa.


Mteja akisha fungua akaunti ya akiba na biashara anunganishwa bure na huduma ya DCB Pesa, huduma mpya ya kufanya miamala ya benki kupitia simu ya mkononi, yaani kuweka na kutoa pesa na kulipia bili mbalimbali. Huduma hii si lazima mteja awe na akunti DCB, bali mtu yeyote mtaani anaweza kujiunga mradi tu awe na namba yoyote ya simu ya mkononi iliyosajiliwa na mojawapo ya kitambulisha cha mpiga kura, utaifa, udereva na paspoti.


Huduma hii inapatikana kwa kupiga *150*85#. Pia Meneja masoko alimueleza Mh. Makinda kuwa huduma za DCB Commercial Bank mbali na Dar es Salaam kwa sasa pia zinapatikana mkoani Dodoma kupitia tawi lake lilifunguliwa hivi karibuni katika jengo la LAPF mtaa wa Makole na mikoa mbali mbali kupitia huduma ya uwakala wa benki yaani DCB Jirani.


Naye afisa wa benki Cecilia Msikula akimuelezea Mh. Makinda huduma ya akiba ya watoto akaunti za watoto –Young saver account ambayo alivutiwa sana nayo hasa Meli ya mtoto, alisema kuwa DCB inatoa huduma hii bila makato ya mwezi ambapo mteja akisha fungua akaunti ya mtoto kwa shi. 5,000 tu anapewa Meli ya Mtoto/ kibubu bure kumjengea mtoto utamaduni wa kujiwekea akiba akiwa bado mdogo kwa ajili ya matumizi yake ya baadaye. Pesa ikisha jaa kwenye Meli ya mtoto yaani kibubu mzazi analeta benki kwa ajili ya kuziweka kwenye akaunti ya mtoto baada ya kuzihesabu.


Katika msafara huo, Spika mstaafu Makinda aliongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa Mh. Jabir Shekimweri.

Spika Mstaafu Anna Makinda akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma.

Spika Mstaafu Anna Makinda akisoma moja ya kipeperushi cha benki ya DCB
katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame


Wananchi wakipatiwa huduma katika banda la benki ya DCB katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mkoani Dodoma.

1 comment: