
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Mbunge wa
Tarime Vijijini, John Heche (kushoto) wakijadiliana jambo mara baada ya
kumaliza kikao kilicholenga kutatua kero za wananchi wanaozunguka mgodi
wa dhahabu wa Acacia NorthMara pamoja na Mgodi husika.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika
kikao na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mkuu wa
wilaya Tarime na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (wa pili kushoto)
kilicholenga kutatua kero wanazokumbana nazo wananchi wanaozunguka
mgodi wa dhahabu wa Acacia NorthMara pamoja na Mgodi husika. Kushoto kwa
Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga. Wa kwanza kulia
Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, Mhandisi
Juma Sementa, Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally
Samaje na Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Leseni,John
Nayopa.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia)
akitembelea maeneo yanayolalamikiwa na wananchi wanaozunguka mgodi wa
dhahabu wa Acacia NorthMara wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani
Tarime. Kulia kwa Waziri ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, na
kulia kwa Mbunge ni Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza
mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Nyakungulu wilayani Tarime ambaye
alikuwa akiwasilisha kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa
Acacia North Mara wakati Profesa Muhongo alipofanya ziara ya kikazi
wilayani Tarime.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia)
akioneshwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga baadhi ya nyumba
zinazodaiwa kutegeshwa kwa ajili ya kulipwa fidia katika moja ya
maeneo yanayozunguka mgodi wa Dhahabu wa Acacia North Mara. Profesa
Muhongo alifika katika eneo la Nyamongo linalozunguka mgodi huo ili
kuzungumza na wananchi na kukagua athari ambazo zinadaiwa kusababishwa
na mgodi katika eneo hilo.
Na Teresia Mhagama, Tarime
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameipa siku 30 Kamati
aliyoiunda ya kutathmini kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu
wa Acacia North Mara ambapo Kamati hiyo inatakiwa kutoa ripoti tarehe
23 Machi 2016.
Kamati
hiyo itakuwa na makundi mawili yatakayofanya kazi sambamba kwa
kuzunguka katika vitongoji tofauti vinavyozunguka mgodi kuanzia tarehe
22 Februari, 2016.
Timu
hiyo itaundwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Sehemu ya
Leseni, Mazingira, Ukaguzi wa Migodi na Idara ya Sheria.
“Wataalam
wengine watakaounda Kamati hii ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Watathmini kutoka Wizara ya Ardhi, Baraza la Usimamizi na
Uhifadhi wa Mazingira ( NEMC) na Wizara ya Maji na Umwagiliaji,” alisema
Profesa Muhongo.
Aliongeza
kuwa Wajumbe wengine ni Wenyeviti wa Vitongoji vitakavyozungukiwa na
Kamati, Wawakilishi wa Mbunge wa Tarime Vijijini, Mgodi wa Acacia North
Mara na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Alisema
kuwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Tarime na Vyombo
vya Usalama wilayani humo havitashiriki katika Kamati husika kwani
baadhi ya tuhuma za wananchi zimeelekezwa katika Ofisi hizo.
Kila
upande unaohusika na zoezi hilo umetakiwa kuwasilisha majina ya wajumbe
wa Kamati kwa Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, siku ya
Jumanne tarehe 16 Februari, 2016.
Alieleza
kuwa Mwenyekiti na Makamu wa Kamati hiyo watatoka Wizara ya Nishati na
Madini na kwamba kamati itafanya kazi katika siku zilizopangwa na si
vinginevyo na mwenendo wa Kazi wa Kamati husika utakuwa ukifuatiliwa
katika kila wiki.
Baada
ya zoezi la upangaji wa Kamati hiyo kukamilika, Mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche, alimshukuru Waziri wa Nishati na Madini na
serikali kwa ujumla kwa kulipa uzito jambo hilo ambalo halijatafutiwa
ufumbuzi kwa miaka kadhaa na kuitakia kamati kila la heri katika
utendaji kazi ili kila mtu apate haki yake anayostahili.
Naye
Meneja Uendelezaji, Mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara, Abel Yiga
kwa niaba ya Mgodi huo amemshukuru Profesa Sospeter Muhongo kwa kufika
wilayani Tarime ili kutatua changamoto kati ya Mgodi na wananchi kwani
wamekuwa wakiwasilisha changamoto zao katika ngazi mbalimbali za uamuzi
lakini utatuzi bado haujapatikana.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga pia ametoa pongezi
kwa Profesa Muhongo kwa kutoa muongozo utakaopelekea kupata suluhisho
la kero zinazowapata wananchi wanaozunguka mgodi pamoja na kero ambazo
mgodi unazipata katika utekelezaji wa majukumu yake.
Alitoa
wito kwa wananchi wilayani Tarime kuwa na imani na Kamati hiyo na kila
upande ukubaliane na taarifa itakayotolewa na Kamati husika.
Baadhi
ya kero zitakazofanyiwa kazi na kamati hiyo ni pamoja na suala la fidia
kwa wananchi waliopisha Mgodi, utegeshaji wa nyumba ndani ya eneo la
Mgodi, athari za mitetemo inayotokana na upasuaji wa miamba, ajira kwa
watanzania ndani ya mgodi, utoaji wa huduma katika mgodi na masuala
mengine yatakayojitokeza wakati zoezi la tathmini litakapoanza.
No comments:
Post a Comment