Mfuko wa Jamii : Mhe. Jenista Mhagama Afunga mkutano wa 25 wa wadau na wanachama wa PPF ,Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 13 February 2016

Mfuko wa Jamii : Mhe. Jenista Mhagama Afunga mkutano wa 25 wa wadau na wanachama wa PPF ,Jijini Dar

 Mgeni rasmi katika Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mkutano huo Meneja wa Rasilimali watu na Utawala wa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT), Sebastian Ndahani Inoshi, mara baara ya kufunga Mkutano huo Februari 12, 2016, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam . Wanaoshuhudia toka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA), Irene Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA, Juma Muhimbi. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
 Mgeni rasmi katika Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba yake ya kufunga mkutano huo, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Washriki wa mkutano huo na Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba fupi ya kufunga mkutano huo iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah akiwakaribisha watoa mada mbalimbali katika Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, uliofanyika kwa mbili, na kufungwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama.
Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kikao cha pili cha Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, unaoendelea kwa siku ya pili, Mkurugenzi Mstaafu wa PPF, Naftali Nsemwa akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya viongozi Waandamizi wa mfuko wa PPF wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mdau Mkubwa wa mifuko ya jamii,Mkurugenzi Mstaafu wa PPF, David Mataka akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, unaoendelea kwa siku ya pili,mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba akizungumza mbele ya Washiriki wa mkutano huo (hawapo pichani) namna ya mfuko huo unavyoweza kutoa huduma kwa jamii na shughuli zake mbalimbali kwa jamii.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akiuliza swali Meza kuu kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko wa PPF hasa kwa huduma yao ya Fao la uzazi
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia Mkutano huo.
Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", uliowakutanisha Wadau mbalimbali, ukiendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment