Michezo / Riadha : Waziri Nape mgeni rasmi Kilimanjaro Marathon. - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


13 Feb 2016

Michezo / Riadha : Waziri Nape mgeni rasmi Kilimanjaro Marathon.


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akielezea jambo alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution ambao ni wadhamini na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marthon  jijini Dar es Salaam. Katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin na kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akifurahia jambo alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution ambao ni wadhamini na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marathon jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia kwa Waziri ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin, Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa na Mkurugenzi Mkuu wa Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle NA Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akikabidhiwa zawadi kutoka TBL kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Lager alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia) na Meneja Masuala ya Nje na Mawasiliano Bibi. Emma Oriyo.
Picha Zote na: Frank Shija, WHUSM.


Na: Frank Shija, WHUSM
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Kilimanjaro Marathoni yatakayofanyika tarehe 28 Februari kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Hayo yamebainisha na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Executive Solution ambayo ndio waratibu wa mbio hizo Bw. Aggrey Marealle walipotembelea ofisini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.

“Mbio za Kili Marathon zinatarajia kufanyika tarehe 28 mwezi huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ambapo mgeni rasmi atakuwa Mhe. Nape Moses Nnauye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo”. Alisema Marealle.

Marealle alisema kuwa Mbio hizo zitakuwa katika makundi manne ambayo ni mbio za Kilomita 42 ambazo ndiyo marathoni yenyewe inayothaminiwa na TBL kupitia bia ya Kilimanjaro,zingine ni Nusu Marathon za kilomita 21 zinazodhaminiwa na Tigo,mbio za kilomita 10 zinazowashirikisha walemavu wanaotumia Baiskeli za matairi matatu na Viti vya matairi zinazodhaminiwa na kampuni ya mafuta ya Gapco na mbio zinginge ni za kilomita 5 ambazo zinadhaminiwa na TBL kupitia kinywajji cha Grand Malt

Aliongeza katika mbio hizo washindi kumi kila kundi watapewa zawadi ambapo mshindi wa kwanza kwa mwanaume na mwanamke katika mbio za kilomita 42 watapatiwa zawadi ya shilingi milioni nne kila mmoja.

Aidha alisema kuwa zaidi ya washiriki 7000 wanakadiriwa kushiriki mbio hizo huku kati yao takribani washiriki 1000 watatoka nje ya nchi.


Kilimanjaro Marathon inatimiza miaka 14 tokea kuanzishwa kwake ambapo waandaji wa mashindano hayo ni Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika Kusini na kuratibiwa na Executive Solutions Ltd ya Tanzania na mdhamini mkuu wa mbio hizo ni Kampuni ya Bia TBL kupitia Bia ya Kilimanjaro Lager.

Post Top Ad