TeknoHama : Wanahabari watakiwa kutumia lugha ya kiswahili kwa Ufasaha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 14 February 2025

TeknoHama : Wanahabari watakiwa kutumia lugha ya kiswahili kwa Ufasaha


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza wakati wa ufuinguzi wa Mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mjini Dodoma.





Karama Kenyunko, Michuzi Tv

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi, amewataka baadhi ya waandishi wa Habari kutumia Kiswahili fasaha wanapohabarisha Umma siyo kuharibu "kubananga" lugha hiyo kuacha.

Akizungumza jijini Dodoma Februari 13,2025 kwenye Mkutano wa mwaka wa Vyombo vya Habari nchini uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Professa Kabudi amesema baadhi ya watangazaji wamekuwa wakipotosha umma kwa kutamka matamshi yasiyo sahihi akitolea mfano apa badala ya hapa, uyu badala ya huyu na wengi huwafuata.

"Tanzania tumefubaza Kiswahili kwa kudumaza kwa maneno kadhaa, kubananga Kiswahili matokeo yake watumiaji wengine wa nchi zinazotuzunguka wanaona hatuzungumzi kwa ufasaha,watangazaji mna jukumu la kuhakikisha mnatangaza kwa lugha fanisi na fasaha kwani ninyi mna mchango mkubwa wa kusahihisha makosa mkiendelea hivyo, hilo ni janga litaigharimu nchi na kuacha kuwa kinara"amesema Kabudi

Amezitaka mamlaka zinahusika kuwachukulia hatua watangazaji ambao hawazingatii maadili ya matamshi ya Lugha fasaha ya Kiswahili.

Sambamba na hilo Profesa Kabudi amevitaka vituo vya utangazaji kutangaza mara kwa mara mabadiliko ya tabia ya nchi ilikuwasaidia wananchi kuishi wa tahadhari badala ya kuweka burudani kwa muda mwingi.

Mkurugenzi wa TCRA Dkt. Jabir Bakari amesema mamlaka imejiwekea utaratibu wa kukutana na vyombo vya habari mara kwa mara ili kupeana taarifa mbalimbali na utekekezaji.

Amesema TCRA ilikuwa ikifanya utafiti wa hali ya utangazaji nchini kutokana na mabadiliko ya teknolojiia ya habari na mawasiliano kwa kuangazia hali ya soko, marejeo ya leseni, mapitio ya ada na wanaangalia namna ya kushusha ada kwa manufaa ya vyombo hivyo na kwamba utafiti huo unatarajia kukamilika Februari 21, 2025.

Amesema baada ya kufanya uchambuzi tayari kwa kuanza utekekezaji anataraji mapendekezo yatakayotolewa kwa serikali kuhusu sera yatafanyiwa kazi haraka.

Bakari amesema pia,wako katika hatua za mwisho kukamilisha mwenendo wa sekta ya mawasiliano ya simu na intaneti, utangazaji na Posta.

Ameongeza changamoto iliyopo ni vituo vingi vya utangazaji kushindwa kuonyesha matumizi na mapato,taarifa za ufadhili na kutoa raia kwa wamiliki kuweka utaratibu wa kuhifadhi takwimu.

Mwakilishi wa wamiliki wa vyombo vya habari kutoka Azam Media Yahaya Mohamed amesema wanaridhishwa sana na mchakato unaoendeshwa na TCRA kuiwezesha sekta ya habari kufanya kazi kwa ubora ila changamoto inayowakabili ni sera na Sheria ya kodi inawabana.

"Tatizo la kodi linatusunbua tumetengeneza mapendekezo kwa tume ya kodi kuwaeleza yale yanayofifisha sekta ya habari, tunatumaini yatafanyiwa kazi,"amesema

No comments:

Post a Comment