Waziri
wa mali asili na utalii Lazaro Nyarandu na waumini mbalimbali baada ya
Ibada ya jumapili Jijini Arusha katika Kanisa la KKKT Diyoyosis ya Mjini
Kati ambapo Waziri Nyarandu alitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi siku
atakayochukua fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya
kuwania Urais kupitia chama cha Mpindunzi .
Waziri
wa mali asili na utalii Lazaro Nyarandu akibadilishana mawazo na Kada wa chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA James Ole Millya baada ya ibada ya
jumapili iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Diyosisi ya mjini kati Arusha
ambapo Nyarandu alitumia nafasi hiyo kutaja rasmi kuwa tarehe 6 mwezi ujao
atachukua fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM
kuwania urais .
Mpiga
picha wa Chanell ten Arusha Aristrides Dotto na Elia Mbonea mwandishi wa
gazeti la Mtanzania wakifanya mahojiano na Waziri wa mali asili na utalii
Lazaro Nyarandu mara baada ya ibada ya jumapili katika Kanisa la
KKKT Diyoyosis ya Mjini kati ambapo Waziri Nyarandu alitumia nafasi hiyo
kutangaza rasmi siku atakayochukua fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa
kupeperusha bendera ya kuwania Urais kupitia chama cha Mpindunzi.
**************
WAZIRI wa Mali Asili na Utalii,
Lazoro Nyalandu ambaye alishatangaza nia ya kukiomba chama Chake cha Mapinduzi
(CCM) kumteua kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, anataraji
kuchukua fomu ya kutimiza adhma yake hiyo Juni 7 mwaka huu mjini Dodoma.
ametangaza rasmi kuchukua fomu ya
kuwania nafasi hiyo baada ya kutangaza nia yake miezi saba iliyopita mkoani Singida.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Arusha jana, Nyalandu ambaye ni Mbunge wa Singida Magharibi,
baada ya kushiriki ibada ya jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa
mjini Kati Arusha.
Nyalandu anaungana na makada
wengine wa CCM kuingia katika kinyang’anyiro hicho ambapo anasema mpango na
dhamira yake ya kuwania kuteuliwa na chama chake uko palepale huku akijinasibu
kuwa dunia itaandika historia pale atakapo ibuka kidedea kwa kupeperusha
bendera ya ccm katika kinyang’anyiro hicho.
“Mpango na dhamira yangu ya kuomba ridhaa ya
Chama change kuniteua kugombea urais mwaka huu upo palepale na dunia itaandika
historia pale nitakapo ibuka kidedea na kuipeperusha bendera ya CCM katika
uchaguzi wa mwaka huu,” alisema Nyalandu.
Waziri Nyalandu atakungana na
makada na Mawaziri wakongwe katika siasa za Tanzania katika kuwania nafasi hiyo
ndani ya CCM kama akina Edward Lowassa, Steven Wasira, Bernard Membe, Samuel
Sitta, na wengineo wengi ambao tayari wameshatangaza nia na dhamira yao ya
kuutaka urais.
No comments:
Post a Comment