Katibu
Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil akizungumza
na kuwapongeza wajumbe wa Kikao Kazi cha Uandaaji wa Mpango wa Ununuzi
na Mpango Kazi wa wizara yake wa mwaka wa fedha 2015/2016 katika kazi
hicho kinachoendelea mjini Morogoro.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi akitoa
mwongozo wa majadiliano kwa Wakuu wa Idara, Maafisa Ununuzi, Maafisa
Bajeti na Wakurugenzi Wasaidizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi kwa mwaka
wa fedha 2014/2015 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi cha
wizara hiyo Mapesi Manyama katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa
Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara wa mwaka wa fedha 2015/2016
kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro. Kushoto ni
Kamishna wa Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga aliyesimama ni
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mapesi Manyama.
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Ununuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Manyama
Mapesi akitoa ufafanuzi wa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi
kwa mwaka wa fedha 2014/2015 wa wizara hiyo, aliyoiwasilisha katika
Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa
wizara wa mwaka wa fedha 2015/2016 kinachoendelea katika hoteli ya Oasis
mjini Morogoro. Wa kwanza kutoka kulia walioketi ni Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi katikati ni Kamishna
wa Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga akifuatiwa na Kamishna wa
Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve.
Mkuu
wa Kitengo cha Ununuzi cha Jeshi la Polisi Asenga akitoa maelezo na
kuwapitisha katika Sheria Mpya ya Ununuzi ya mwaka 2011 katika Taasisi
za Umma wajumbe wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na
Mpango Kazi wa mwaka wa fedha 2015/2016 wa wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi. Mapitio hayo yamefanyika katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa
Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara wa mwaka wa fedha 2015/2016
kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sheria na Usajili wa Vyama Marlin Komba katika wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya
Kisheria kuhusu masuala ya Ununuzi katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa
Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
wa mwaka 2015/2016 kinachowahusisha Maafisa Bajeti, Maafisa Ununuzi,
Wakurugezi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Taasisi zote za wizara
hiyo kinachoendelea katika hoteli ya Oasisi mjini Morogoro ,
Wanaomsikiliza ni baadhi ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Jeshi la
Polisi na Uhamiaji.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Haji
Janabi akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Kifedha yanayohusu
Ununuzi katika Taasisi za Umma katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa
Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa mwaka wa fedha 2015/2016 wa wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kikao kinachoendelea katika hoteli ya Oasis
mjini Morogoro.
Mrakibu
Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Fane Kapinga akiwasilisha Mada kuhusu
Uandaaji wa Mpango wa Ununuzi wa Mwaka wa Fedha wa 2015/2016 kwa
kutumia Majedwali yaliyoainishwa na Wakala wa Ununuzi Serikalini (PPRA)
katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa mwaka 2015/2016
kinachowahusisha Maafisa Bajeti, Maafisa Ununuzi, Wakurugezi,
Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Taasisi zote za wizara hiyo
kinachoendelea katika hoteli ya Oasisi mjini Morogoro.
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Lilian Mapfa akifuatilia kwa makini ufafanuzi wa Sheria Mpya
ya Ununuzi ya mwaka 2011 katika Taasisi za Umma wakati Mkuu wa Kitengo
cha Ununuzi cha Jeshi la Polisi Mathew Asenga akitoa maelezo na
kuwapitisha katika Sheria Mpya ya Ununuzi ya mwaka 2011 katika Taasisi
za Umma wajumbe wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na
Mpango Kazi wa mwaka wa fedha 2015/2016 wa wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro.
Kamishna
wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Makame wa kwanza kutoka kulia
akifuatiwa na Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji TRITA mjini Moshi John Choma na
watatu kutoka kulia ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Idara ya
Uhamiaji Piniel Mgonja wakimsikiliza kwa Makini Mkurugenzi wa Kitengo
cha Ununuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Manyama Mapesi wakati
akitoa ufafanuzi wa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi kwa
mwaka wa fedha 2014/2015 wa wizara hiyo, aliyoiwasilisha katika Kikao
Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara wa
mwaka wa fedha 2015/2016 kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini
Morogoro.
No comments:
Post a Comment