Kampuni
ya mafuta na gesi ya Swala (Tanzania) Plc ("swala" au "Kampuni") inayo
furaha kutangaza kwamba imefikia makubaliano ya kugawana umiliki na
Kampuni ya Tata Petrodyne Limited ("TPL"), kampuni ambayo ni sehemu ya
Kampuni ya Kimataifa ya Tata sons Limited, ambapo TPL itakuwa ikifanya
shughuli zake kwenye maeneo ya leseni ya Pangani na Kilosa-Kilombero
nchini Tanzania. Hii itaiwezesha Kampuni ya swala kubaki kwenye maeneo
yake ya leseni na ili kupata fedha kwa ajili ya shughuli za utafutaji
hapo baadaye katika njia ambayo itapunguza hasara kwa wanahisa wake wa
sasa.
Kampuni
ya Tata Sons Limited ni Mratibu wa uendeshaji wa shughuli kubwa za
makampuni ya Tata na kumiliki hisa zote muhimu kwenye makampuni haya, na
kwa kawaida inajulikana kama kundi la Tata (Tata Group). Kundi la Tata
lina mtaji wa soko wa takribani dola za Kimarekani bilioni 110 na
inawakilisha zaidi ya asilimia 8 ya jumla ya mtaji wa soko katika soko
la hisa la Bombay.
Katika
sekta ya mafuta na gesi, makubaliano ya kugawiana umiliki ni
makubaliano yaliyoingiwa kwa mmiliki wa leseni moja au zaidi (anayegawa
umiliki huo) na kampuni nyingine ambayo inataka kupata asilimia ya
umiliki wa leseni hiyo kwa ajili ya kutoa huduma (na 'kujimilikisha).
Makubaliano ya kugawana umiliki yanatofautiana na shughuli za kawaida
kati ya wakodishaji wawili wa mafuta na gesi, kwa sababu cha msingi
kuzingatia ni utoaji wa huduma, badala ya ubadilishaji rahisi wa fedha.
Makubaliano yaliyofikiwa na TPL:
• Baada
ya kupokea vibali vya kiserikali kwa ajili ya uhamisho wa maslahi,
kampuni ya TPL itailipa kampuni ya swala Jumla ya dola za kimarekani
milioni 5.7 kwa ajili ya usawa wa maslahi, asilimia 25 katika leseni ya
Kilosa-Kilombero na usawa wa maslahi wa asilimia 25 katika leseni ya
Pangani kama fidia zidi ya gharama zilizotumika zamani kwenye leseni;
• Kampuni
ya TPL itaibeba Swala kwa gharama ya kisima cha awali kwenye leseni ya
Kilosa-Kilombero, hadi kiwango cha juu cha dola za kimarekani milioni
2.5 (swala inakadiria gharama za awali za kisima kuwa dola za kimarekani
milioni 10.0);
• Kampuni
ya TPL itaibeba Swala kwa gharama ya kisima cha awali kwenye leseni ya
Kilosa-Kilombero, hadi kiwango cha juu cha dola za kimarekani milioni
2.125 (swala inakadiria gharama za awali za kisima kuwa dola za
kimarekani milioni 8.5);
• Kampuni
ya TPL itailipa swala zaidi ya dola za kimarekani milioni 1.0 dhidi ya
gharama ya kisima cha pili kufuatia ugunduzi wa kibiashara katika kisima
cha awali kwenye leseni ya Kilosa-Kilombero. Gharama zilizotumika zaidi
ya kiasi hiki zitabebwa na washirika kulingana na usawa wao.
• Kwenye ukamilisho wa Muamala uliotangazwa leo, usawa katika leseni mbili utakuwa:
Swala TPL * Otto
Kilosa-Kilombero 25% 25% 50%
Pangani 25% 25% 50%
* Otto Energy (Tanzania) Pty Ltd “(Otto”) ni mmiliki mkubwa wa sehemu ya Otto Energy Ltd (ASX: OEL)
Kampuni
inakadiria kuwa kwa sasa imejidhatiti kikamilifu kwa majukumu yake
yaliyobakia kwenye leseni zote mbili. Kampuni ya swala ilishauriwa
katika shughuli hii na kampuni ya First Energy Capital ("FIRSTENERGY")
na kampuni ya TPL ilishauriwa na benki ya Rand Merchant.
Naye
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Swala Dk David Mestres Ridge alisema:
"Kampuni inayo furaha kutangaza makubaliano ya swala Tanzania na kampuni
ya TPL inayofahamika kwa sifa nzuri. Ugawaji huu wa umiliki utatoa
mwanya kwa Kampuni kufadhili majukumu yake iliyojiwekea kwa njia ambayo
inapunguza hatari kwa wanahisa wetu bila kuwa na haja ya kuongeza hisa
ya ziada za kianzio kwa wakati huu.
Napenda
kutoa shukurani kwa FirstEnergy kwa ajili ya mbinu zao za kitaalamu
katika kuendesha mchakato wa kugawa umiliki na kwa ajili ya kuzalisha
riba kutoka kwenye makundi hayo yanayoheshimika sana.
Kwa
sasa kampuni ya Swala itazingatia kupata ridhaa muhimu na vibali vya
kiserikali ili kuruhusu ubia mpya uliotengenezwa ili kuendeleza mipango
ya uchimbaji kwenye leseni zote mbili na tunataraji kuboresha soko
pamoja na mwongozo wa lini mambo haya yaanze.
No comments:
Post a Comment