Naibu kamishna wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani SACP Johanes Kahatano(katikati) akiwafafanulia jambo Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kushoto) Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi wa Polisi Mohamed Mpinga, Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga kuhusiana na kampeni ya kuzuia ajali barabarani inayojulikana kama“Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” kupitia namba 0800757575.Kampeni
hiyo inaendeshwa na jeshi la polisi kikosi cha Usalama
barabarani,Vodacom Tanzania na kwa vyombo vya habari vya kampuni ya IPP .
Mkuu wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) kuhusiana na kampeni ya kuzuia ajali barabarani inayojulikana kama“Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” kupitia namba 0800757575,Katikati ni Mkurugenzi
wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga.Kampeni hiyo inaendeshwa na
jeshi la polisi kikosi cha Usalama barabarani,Vodacom Tanzania na
Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni ya IPP .
Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga(katikati)akishuhudiwa na Mkuu wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga(kushoto) Rosalynn Mworia Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania akibandika stika yenye namba 0800757575 ambayo
imetolewa mahususi kwa abiria wanaotumia vyombo vya moto kusafiria
kutoa taarifa bure kupitia namba hizo wakati wa uzinduzi wa kampeni
inayojulikana kama “Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” Kampeni hiyo
inaendeshwa kwa usirikiano baina ya Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama
barabarani,Vodacom Tanzania na vyomo vya habari vinavyomilikwa na
kampuni ya IPP
Wananchi watakiwa kutoa taarifa za ukiukaji wa kanuni na sheria za usalama barabarani
· Ni kupitia kampeni ya zuia ajali sasa,toa taarifa mapema
Dar es Salaam, Mei 27, 2015: Kufuatia
wimbi la ajali lililosababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu wengine
kujeruhiwa,wananchi wametakiwa kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali
nchini kwa kutoa taarifa kwa vyombo ya usalama waonapo kanuni na sheria
za barabarani zinakiukwa na madereva wazembe hasa wanapokuwa wanasafiri
na magari yaendayo masafa marefu.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna
Msaidizi wa Polisi Mohamed Mpinga wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya
kuhamasisha usalama barabarani ijulikanayo kama “Zuia Ajali Sasa,Toa
Taarifa Mapema” inayofanyika
kwa ushirikiano wa serikali kupitia Jeshi la Polisi, kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom na kampuni ya vyombo vya habari vya IPP. Uzinduzi
huo umeambatana na kuzinduliwa na namba maalumu ya kutoa taarifa za
ukiukwaji wa kanuni na usalama barabarani ambayo ni: 0800757575.
“Matukio
ya ajali hapa nchini yatapungua iwapo watumaji wa barabara hususan
madereva watazingatia sheria na kanuni za usalama baabarani na ni jukumu
letu sote kuvalia njuga tatizo hili na kutoa taarifa za madereva na
watumiaji wa barabara wazembe kwa vyombo vinavyohusika ili wachukuliwe
hatua za kisheria. Nayapongeza makampuni ya Vodacom na IPP Media kwa
kuungana na Jeshi la Polisi katika kampeni hizi,” alisema Kamanda
Mpinga.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkuu wa Mawasiliano ya makampuni na
Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia amesema “Tukiwa kampuni ya
mawasiliano tutaendelea kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali nchini
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walioko katika mapambano haya. Leo
tumetoa namba ya simu ya kutoa taarifa za ukiukwaji wa sheria barabarani
ambayo ni ya bure kwa wateja wa Vodacom.
Mteja
atakayepiga kutoa taarifa kupitia namba hii hatatozwa gharama zozote
bali tutazibeba ikiwa moja ya jitihada za kuunga mkono kampeni hizi.
Nawakumbusha watumiaji wa barabara tuzingatie sheria na kanuni na
tusisite kutoa taarifa kwa vyombo husika tunapoona vitendo vya
kuhatarisha maisha kutoka kwa watumiaji wa barabara wazembe,” alisema.
Vodacom
imekuwa mstari wa mbele katika kampeni za uhamasishaji usalama
barabarani na mwaka jana ilizindua kampeni ya “Wait to Send”
inayohamasisha madereva kutotumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha
vyombo vya moto na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.
Wakati
wa uzinduzi wa kampeni hii uliofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo
mikoani cha Ubungo ambapo madereva waligawiwa pete maalumu za
kuwakumbusha kuacha matumizi ya simu wanapokuwa wanaendesha vyombo vya
moto, pia waligawiwa vipeperushi ya kuwakumbusha kanuni na sheria za
usalama barabarani. Pia abiria walihimizwa kutoa taarifa za uzembe wa
madereva wanapokuwa safarini kupita vibandiko vyenye ujumbe wa kampeni
hii usemao “Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” vyenye namba ya kutoa taarifa ya: 0800757575..
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga
alisema kuwa kampeni hii muhimu ina uwezo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa
nap engine kutokomeza kabisa kupitia teknolojia za mawasiliano.
“Kampeni tunayoizindua leo itahusisha kurushwa kwa taarifa na matukio ya
ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani kupitia Radio One Stereo, ITV
na Capital Radio. Kusudi kubwa la kufanya hivi ni kuendeleza ujumbe wa
usalama barabarani ka upana zaidi na pia kuwaweka bayana wale wote
wanaokiuka na kuvunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi kabisa.
Tutatumia pia uwepo wetu katika mtandao kupitia Twitter na Facebook
katika kuhakikisha tunatumia kila nafasi kusambaza ujumbe huu muhimu,” alisema Rweyunga.
Aliongeza
kuwa ushirikiano kati ya vyombo vyao vya habari na Vodacom Tanzania
utafanikiwa na kuchangia kwa kiasi kikubwa kampeni hii ya uhamasishaji
wa umma. Kujitolea kwa vyombo hivi vya habari kutaisaidia kampeni hii
kufikia malengo yake yote, kubwa haswa likiwa kufanya barabara kuwa njia
salama kuliko zote za usafiri.
No comments:
Post a Comment