Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Liberata Mulamula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Balozi
Mulamula anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kuongoza Wizara hiyo na
kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Hafla
hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
akishuhudia Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Mulamula akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya
kumwapisha.
|
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mulamula Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Hassan Simba Yahya kuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa. Kabla ya uteuzi huo Balozi Yahya alikuwa Mkurugenzi wa Idara
ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei,
2015.
|
Mhe.
Rais Kikwete akishuhudia Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya akisaini Hati ya Kiapo
mara baada ya kumwapisha.
|
Mhe.
Rais Kikwete akimpongeza Balozi Yahya mara baada ya kumwapisha kuwa
Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
akimwapisha, Mhe. Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi
Arabia. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mgaza alikuwa Afisa Mambo ya Nje
Mkuu na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
|
Rais Kikwete akishuhudia Balozi Mgaza akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha.
|
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mgaza Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
|
Mhe.
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi
Yahya na Balozi Mgaza mara baada ya kuwaapisha katika nyadhifa zao mpya
|
Mhe.
Rais Kikwete kwa pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe.Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa nne kushoto), Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)
(wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (wa tatu kutoka kulia),
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kutoka kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya na Balozi
Mgaza muda mfupi baada ya kuapishwa.
|
Mhe.
Rais Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na Balozi Mulamula, Balozi
Yahya, Balozi Mgaza na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mabalozi wa Tanzania.
|
Mhe.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi aliowaapisha pamoja na
baadhi ya Wakurugenzi wa Idara za Mambo ya Nje na Watumishi wa Wizara
hiyo
|
Mhe.
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula (kushoto)
na mumewe, Bw. George Mulamula (kulia). Picha na Reginald Philip
|
No comments:
Post a Comment