Pichani
ni Mgombea anayetajwa kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Arusha
mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Thomas Munisi
Na Pamela Mollel, Jamiiblog.co.tzMgombea anayetajwa kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Arusha mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Thomas Munisi amewataka wagombea wa chama hicho kutochafuana kwenye majukwaa na vijiwe bali wafanye kampeni za kistaarabu.
Munisi,ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Kilimanjaro Millenium Printers(KPML) yenye makao makuu yake jijini Arusha alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuhusu uamuzi wake wa kugombea ama la.
Hadi sasa jijini Arusha jumla ya wagombea saba wamejitokeza kutia nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupitia CCM ambao ni Kim Fute,Mustapha Panju”Bushbuck”,Phillemon Mollel”Monaban”,Victor Njau,Edmund Mgemela,David Rwenyagira pamoja na mbunge wa zamani wa jimbo hilo Felix Mrema.
Akiongea katika hoteli ya Palace iliyopo jijini Arusha alisema kuwa si vyema wagombea wa CCM kuanza kampeni za kuchafuana kupitia kwenye vijiwe na majukwaa kwa kuwa haileti picha nzuri ndani ya chama.
“Mimi nashangaa wagombea wanapita huko vijiweni na kuanza kuchafua wenzao wakati sote tunajenga nyumba moja”alisema Munisi ambaye pia ni mmiliki wa kamuni ya madini ya Tom Gems
Hatahivyo,alisema kuwa ndani ya CCM watajitokeza wagombea mbalimbali lakini mwisho wa siku ni mgombea mmoja tu atakayepitishwa na chama kwa lengo la kupeperusha bendera ya CCM.
Akizungumzia uamuzi wake wa kugombea jimbo hilo au la alisema kuwa kwa kuwa taratibu ndani ya chama zimeshatangazwa na muda ukiwadi atafanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya wakazi wa jimbo la Arusha mjini.
“Chama kimeshatangaza taratibu ninachokifanya ni kusubiri muda ufike nitafanya maamzi lakini kwa sasa naheshimu kanuni za chama”alisema Munisi
Munisi,ni miongoni mwa vijana wanaotajwa “kulimezea mate”jimbo la Arusha mjini linaloshikiliwa na mbunge wa sasa wa jimbo hilo,Godbless Lema kupitia Chadema ambaye naye tayari ameshatangaza kurudi kwenye kinyang”anyiro cha kugombea kwa mara nyingine.
No comments:
Post a Comment