Mfuko wa Jamii : PPF Yawapa Tuzo Wafanyakazi wake Bora wa Mwaka 2014 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 17 May 2015

Mfuko wa Jamii : PPF Yawapa Tuzo Wafanyakazi wake Bora wa Mwaka 2014

Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Martin Mmari, (kushoto), akimkabidhi cheti Mfanyakazi bora wa Mfuko huo kutoka kanda ya Ziwa, Bernard Kyaduma, wakati wa hafla ya kuwapatia tuzo wafanyakazi bora wa Mfuko huo mwaka 2014.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Julius Kam Mganga, (wapili kushoto), akitunuku cheti Mfanyakazi bora wa jumla wa Mfuko huo kwa mwaka 2014, Angelina Napacho kutoka kurugenzi ya Operesheni ya Mfuko huo, wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi bora kutoka kila idara kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumapili Mei 17, 2015. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani, Hoseah Kashimba, na Mkurugenzi wa Fedha, Martin Mmari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Julius Kam Mganga, akitoa hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, William Erio.
Kamati ya maandalizi ya sherehe hoyo, chini ya uenyekiti wake, Mratibu wa Ofisi za Kanda za PPF, Mbaruku Magawa Mbaruku, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla hiyo.
Mfanyakazi bora wa mwaka wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Angelina Napacho, akiwa na uso wa furaha huku akiwa amebeba maua na kadi za kumpongeza wakati wa hafla hiyo.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba, akitumbuiza kwenye hafla hiyo.
Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe, (kushoto), akisakata dansi na mfanyakazi mwenzake kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa TUICO wa wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akitoa nasaha zake.
Nancy Warioba, (kushoto), mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kutoka kitengo cha mifumo ya computa (IT), akipongezwa na mfanayakzi mwenzake baada ya kuibuka mfanyakazi wa bora wa mwaka 2014, wakati wa sherehe ya kuwatuza wafanyakazi bora wa mfuko huo kutoka kila idara, hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili Mei 17, 2015. Angelina Napacho kutoka kurugenzi ya Operesheni ya Mfuko huo, ndio aliibuka mfanyakzi bora wa jumla.
Mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kutoka kurugenzi ya huduma za kisheria ya Mfuko huo, Nyambilila Ndoboka, (kushoto0, akipongezwa na wenzake baada ya kupewa tunzo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Julius Kam Mganga, (katikati), na wakurugenzi wengine, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa mwak 2014 wa Mfuko huo kutoka kila idara, baada ya kuwatunuku vyeti kwenye hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia Jumapili Mei 17, 2015.

No comments:

Post a Comment