Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na
Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kushoto) akizungumza na
wandishi wa Habari (pichani hawapo) baada ya hitimisho la Mkutano wa
nne wa mafunzo ya Upasuaji wa Ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya
fahamu, Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dkt Seif Rashid, uliomalizika hivi karibuni. ambapo wakishirikiana na
Wataalamu madaktari bingwa wa Chuo cha Weill Cornell toka Marekani
kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya kisasa, ambapo
Watanzania 21 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo wakishirikiana na
madaktari toka Tanzania , Uganda, Rwanda, Southi Afrika, Marekani na
Ulaya. Dokta Othman Kiloloma, alimshukuru Rais Jakaya Kikwete ambaye
aliye waweka karibu na wenzao wa Chuo cha Marekani na kuwashukuru wenzao
wa chuo cha marekani kwa kuwawezesha kufanyika upasuaji huo. (wakwanza
kulia) ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa
ya fahamu Dk.Hamisi Shabani,ambaye aliwaeleza waandishi hao kua mgonjwa
mmoja kufanyiwa upasuaji anagharimu kiasi cha dola elfu moja za upasuaji
huo nahaihusiani na mambo mengine.na katikati ni Profesa Philip Steg
toka Chuo cha Marekani nayeye alipata nafasi ya kuongea na waandishi hao
na kuwashukuru Wataalamu wa Moi (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa
Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (wapili) kushoto
na kuanzia kulia ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo
na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani anaye fatia ni Profesa Philip
Steg toka Chuo cha Weill Cornell Marekani na kushoto ni Menneja ea
Taasisi ta Moi Almas Jumaa.
Madaktari wakiwakatika Upasuaji na ikiongozwa Dk, Japhet Ngerageza
Mashine
ya kisasa yenye thamani shilingi mil. 700 iliyotolewa msaada na Weill
Cornell toka Marekani ikikumika kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania kwa
Muungano wa jitihada za Rais Jakaya Kikwete
Madaktari
Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu
(MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa wa Chuo cha Weill Cornell toka
Marekani kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo
wagonjwa 21 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo. Dar es Salaam
Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa
ya Fahamu (MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa wa Chuo cha Weill
Cornell toka Marekani wakionyeshana jambo wakati walipokuwa wafanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya
kisasa ambapo wagonjwa 21 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo. Dar
es Salaam
Madaktari wakiwa katika chumba cha Upasuaji
No comments:
Post a Comment