Mkurugenzi
Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen. Mbazi Msuya
akimpongeza Nahodha wa meli ya Mv. Liemba, Mande Mangapi mara baada ya
kuwafikisha salama waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wapatao
600, katika bandari ya Kigoma kutoka Kagunga, saa mbili usiku tarehe 15
Mei 2015, kushoto ni Kaimu Katibu Tawala mkoani Kigoma, Salvatory
Shauri.
Ujumbe
uliongozwa na Mkurugenzi Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
Brig.Jen. Mbazi Msuya ukiwa katika bandari ya Kigoma kwa ajili ya
kuwapokea waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya
kuwasili kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya Mv. Liemba saa mbili
usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Baadhi
ya waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwasili katika bandari
ya Kigoma kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya Mv. Liemba saa mbili
usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Askari
wa Jeshi la Polisi, Konstebo Genovefa Kizinza akifanya ukaguzi wa mzigo
aliowasili nao muomba hifadhi ya Ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya
kuwasili katika bandari ya Kigoma kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya
Mv. Liemba saa mbili usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Baadhi
ya waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi wakiwa wamejipanga tayari
kusafirishwa kwa mabasi hadi kwenye kambi ya mpito ya Lake Tanganyika
muomba hifadhi ya Ukimbizi kutoka Burundi mara baada ya kuwasili katika
bandari ya Kigoma kutoka kijiji cha Kagunga na Meli ya Mv. Liemba saa
mbili usiku, tarehe 15 Mei 2015.
Mkurugenzi
Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen. Mbazi Msuya
(katikati) akiwa na Uongozi wa mkoa na baadhi ya wawakilishi wa
mashirika ya kimataifa yanayohudumia wakimbizi mara baada ya kuwapokea
waomba hifadhi ya ukimbizi kutoka Burundi katika bandari ya Kigoma
kutoka Kagunga, saa mbili usiku tarehe 15 Mei 2015, (mwenye tai) ni
Kaimu Katibu Tawala mkoani Kigoma, Salvatory Shauri.
No comments:
Post a Comment