Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifunga Semina ya
Siku Nne ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na watendaji Wakuu
wa Serikali juu ya uchambuzi wa Bajeti na Masuala ya Uchumi iliyokuwa
ikifanyika katika ukumbi wa Z. Ocean Hoteli Chuwini Wilaya ya Magharibi
“A”.
Baadhi
ya Wajumbne wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotub a ya Balozi
Seif hayupo pichani wakati akiifunga semina ya uchamguzi wa Bajeti na
masuala yua Uchumi.
Waziri
wa Fedha ZanzibarMh. Omar Yussuf kulia na Waziri wa Biashara, Viwanda
na Masoko Mh. Nassor Ahmed Mazrui wakiwa makini kufutailia Hotuba ya
Balozi Seif kwenye Semina yao.
Baadhi
ya Watendaji Wakuu wa Serikali ambao wameshiriki Semina ya uchambuzi wa
Bajeti na masuala ya Uchumi hapo Z. Ocean Hoteli Chuwini Wilaya ya
Magharibi “ A “.
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Pandu Ameir Kificho Kulia na
Waziri wa Nchi Ikulu na Utawala Bora Dr. Mwinyihaji Makame wakikamilisha
Semina hayo ya uchambuzi wa Bajeti na masuala ya Uchumi. Picha na -
OMPR – ZNZ.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema yapo
matumaini makubwa ya kukua kwa Uchumi wa Zanzibar kukua ambako
kutategemea pia Uchaguzi Mkuu wa Mwezi wa Oktoba mwaka huu kama
utakwenda kwa amani na utulivu.
Alisema
Serikali kwa upande wake itahakikisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar
inaendesha Uchaguzi wenye uwazi, huru na haki kwa wagombea wote
watakaobahatika kushiriki kwenye uchaguzi huo.
Balozi
Seif Ali Iddi akiwa kiongozi wa shughuli za Serikali alisema hayo
wakati akiifunga Semina ya siku Nne ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
pamoja na watendaji Wakuu wa Serikali juu ya uchambuzi wa Bajeti na
Masuala ya Uchumi iliyokuwa ikifanyika katika ukumbi wa Z Ocean Hoteli
Chuwini Wilaya ya Magharibi “A”.
Alisema
Uchaguzi ulio salama na haki utakuwa kichocheo kikubwa kitakachotoa
fursa ya kusaidia kukua kwa uchumi wa Taifa sambamba na kuhamasiha
wawekezaji wengi zaidi kumiminika nchini kwa lengo la kuwekeza miradi
yao ya Kiuchumi.
Balozi
Seif aliwanasihi wanasiasa ni vyema wakajiepusha na kauli za kuchochea
vurugu, huku akiwataka wananchi kutokubali kuchochewa kuanzisha fujo
wakati Waandishi wa Habari wakawajibika ipasavyo kutekeleza majukumu yao
kwa jamii katika misingi ya uadilifu.
Akizungumzia
Bajeti inayozingatia matokeo { PBB } ambao ni mfumo mpya utakaotumika
katika majadiliano ya Baraza la Wawakilishi kwenye Bajeti ya mwaka huu
Balozi Seif alisema mfumo huu utawasaidia Wananchi kuelewa kwa uwazi
Bajeti ya Serikali yao na imeleta matokeo gani kwao.
Alisema
Mfumo huu mpya ambao utawapa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuendelea
kujifunza unasaidia kujenga uwazi katika suala zima la matumizi ya
Serikali jambo ambalo ni muhimu katika jitihada za kukuza uchumi wa
Wananchi.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
17/5/2015.
No comments:
Post a Comment