-
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwakaribisha wageni katika hafla ya
ufunguzi wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi kwa waajiriwa wapya Leo Jijini
Dar es Salaam.
Mkuu
wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni
Rasmi katika ufunguzi wa Mafunzo hayo na kuwataka washiriki kushiriki
kikamilifu kwenye kipindi cha mafunzo ili waweze kuwa na mbinu thabiti
za ukusanyaji kodi kwa maslahi ya Taifa
Naibu
Mkurugenzi kitengo cha Rasilimali Watu Bw. Victor Kimaro akiwaeleza
washiriki wa Mafunzo namna mchakato ulivyofanyika na kuwataka
kuthibitisha ubora wao katika kipindi chote cha mafunzo
- Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Bw. Rished BADE akiongea na washiriki wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi na
kuwataka kufanya kazi kama watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na
kutumia fursa hiyo kujiimarisha kiutendaji kabla ya kuanza kazi rasmi ya
ukusanyaji kodi inayohitaji uadilifu na ueledi wa hali ya juu katika
kuitekeleza, wakati wa hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia)
akikata utepe kwenye boksi lililokuwa na Mtaala utakaotumia katika
mafunzo hayo wakati wa ufunguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia)
akionesha mtaala utakaotumika katika mafunzo ya washiriki 150
waliodahiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade(wa sita kutoka Kulia) na Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi Prof. Isaya Jairo (ITA) (wa Tano kutoka kushoto) wakiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Mafunzo hayo baada ya kuyazindua leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment