MKUU
wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda akiwa anafungua mkutano ulioandaliwa
na mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF kwa wadau wake jijini
Arusha uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya
kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo.(Habari Picha na
Pamela Mollel wa http://jamiiblog.co.tz/)
Meneja
masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina akizungumza katika mkutano
na wadau kutoka sekta mbalimbali uliofanyika jijini Arusha uliolenga
kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF)
sambamba na mabadiliko katika mfuko huo.
MKUU
wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda akiwa anasoma kipeperushi chenye
maelezo kuhusu mfuko wa GEPF,kushoto Meneja masoko wa mfuko wa GEPF
Aloyce Ntukamazina,kulia ni meneja kanda ya kaskazini Dennis Kaitwa
Kushoto Mwalimu Jonuis Lowassa kutoka idara ya utumishi wa walimu(KTSD)wilaya ya Mounduli na Longido
Afisa masoko GEPF Clement Oning'o ambaye alikuwa Mc wa shughuli hiyo akitoa utaratibu katika mkutano huo
Afisa muajiri Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Siraji Msophe akifurahia jambo katika mkutano huo
MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda wakiwa wanateta jambo na Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina
Wadau wakiwa katika mkutano huo
Kushoto
Afisa rasilimali watu na utawala Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani
Kilimanjaro Isaial Bayege akiwa ananukuu baadhi ya mambo katika mkutano
huo ulioandaliwa na mfuko wa GEPF jijini Arusha
Kulia ni Afisa Rasilimali watu katika chuo cha Nelson Mandela Bi.Honorina Mashingia
Meneja
masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina akizungumza na waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu mfuko wa GEPF jijini Arusha
Meneja kanda ya kaskazini kutoka mfuko wa GEPF Dennis Kaitwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha
Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya Pamoja na mgeni Rasmi MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda
MKUU wa
mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda ameitaka mifuko ya jamii kuendelea kutoa
elimu zaidi kwa wananchi kujiunga na mifuko hiyo ili kuweka akiba ambayo
itasawasaidia kwa maisha yao ya baadaye.
Aliyasema
hayo wakati akizungumza katika mkutano wa wadau kutoka sekta mbalimbali
uliofanyika mjini hapa uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko
wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo
.
Alisema
kuwa, mifuko hiyo ina manufaa makubwa sana kwa jamii hususan kipindi cha
kustaafu ambacho huwa ni kipindi kigumu sana kwa asilimia kubwa ya
wastaafu ambapo wengi wao mifuko hiyo huwasaidia sana kuondokana na
maisha magumu yanayowakabili.
Ntibenda
alisema kuwa, kuna idadi kubwa sana ya wastaafu ambao wangependa
kujiunga na mifuko hiyo ila kinachowawia ugumu ni kutopata elimu ya
kutosha juu ya kujiunga na mifuko hiyo ambayo ina manufaa makubwa sana
kwao.
Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina alisema
kuwa ,mfuko huo umeanza kutoa elimu nchi nzima juu ya mabadiliko ya
mfuko huo ambapo wamezindua mafao mapya manne ambayo ni fao la
elimu,uzazi,fao la kuanza maisha ,na fao la kujikimu ambapo mafao hayo
yote ni yataanza kutumika katika mfuko huo hivi sasa.
Aloyce
amesema kuwa,mfuko huo wamekuwa wakijitahidi sana na kukabiliana na
changamoto ya wajiri kutofikisha mafao ya wafanyakazi kwenye mifuko kwa
wakati ambapo mfuko huo wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha makato hayo
yanafika kwa wakati na muda ulipangwa .
Aidha
washiriki wa mkutano huo, wakizungumza kwa nyakati tofauti waliutaka
usimamizi wa mifuko hiyo kuongeza mifuko zaidi ili wananchi wawe katika
hali nzuri ya kiuchumi kwa kutumia mifuko mbalimbali na kuondokana na
kusongamana kwenye mifuko michache iliyopo .
Meneja wa
mfuko huo kanda ya kaskazini ,Denis Kaitwa amesema kuwa wamekuwa
wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kutoa elimu kutokana na asilimia
kubwa ya wananchi kuwa wagumu kujiunga na mifuko hiyo ambayo ina manufaa
makubwa kwa maisha yao.
Kaitwa
alisema kuwa,kupitia mkutano huo utawawezesha wadau hao kutoa elimu
zaidi kwa wafanyakazi wao na hatimaye kuweza kutambua umuhimu wa
kujiunga na mfuko huo wa GEPF ambao una manufaa makubwa kwa jamii.
No comments:
Post a Comment