Matukio : Waziri Lukuvi Aanza Ziara yake Jijini Mwanza - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 12 March 2015

Matukio : Waziri Lukuvi Aanza Ziara yake Jijini Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akitoa maelezo ya hali ya migogoro ya Ardhi iliyopo Mkoani Mwanza kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi alipokutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa katika ziara yake Mkoani Mwanza.Picha na Muungano Saguya- Mwanza
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mh. Jaji Mfawidhi Makalamba alipokutana naye ofisini kwa Jaji huyo Jijini Mwanza ili kupata namna bora ambayo mhimili wa mahakama unaweza kusaidia kutatua migogoro ya ardhi nchini. Waziri Lukuvi yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Mwanza yenye nia ya kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Jijini Mwanza Mh. Makaramba na watendaji wa sekta ya ardhi na mahakama alipomaliza mazungumzo na Jaji huyo jana.

No comments:

Post a Comment