Miundombinu : Kamati ya Bunge ya Miundombinu Yatembelea Ofisi za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 12 March 2015

Miundombinu : Kamati ya Bunge ya Miundombinu Yatembelea Ofisi za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya akizungumza na watendaji wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za Serikali, wakati walipotembelea ofisi za Wakala jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga akiwaongoza wajumbe Kamati ya Bunge ya Miundombinu kkwenda kukagua nyumba zinazojengwa kwa ajili ya watumishi wa Serikali eneo la Mabwepande, Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Juma Kapuya akipewa ufafanuzi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga, wakati Kamati hiyo ilipotembelea nyumba za Serikali na kuona utekelezaji wake.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga akiwaonesha baadhi ya nyumba ambazo zinajengwa na TBA (hazipo pichani)kwa ajili ya watumishi wa Serikali.
Baadhi ya nyumba za watumishi wa Serikali zinazojengwa na TBA eneo la Mabwepande.

No comments:

Post a Comment