Nishati Zetu : Dk. Ali Mohamed Shein Azindua mradi wa Umeme Kijiji cha Dongongwe kati ,Unguja - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 19 December 2014

Nishati Zetu : Dk. Ali Mohamed Shein Azindua mradi wa Umeme Kijiji cha Dongongwe kati ,Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC) Hassan Ali Mbarouk wakati alipofika Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja kuzindua Nishati ya Umeme.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza wakati alipofika Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja kuzindua Nishati ya Umeme.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC) Hassan Ali Mbarouk (katikati) wakati alipofika Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja kuzindua Nishati ya Umeme (kulia)Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban (wa pili kulia) Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua Nishati ya Umeme Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija (kutoka kulia) Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib na Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC) Hassan Ali Mbarouk.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiingiza namba katika fungua pazia kuzindua Nishati ya Umeme Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija (kutoka kulia) Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib na Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC) Hassan Ali Mbarouk.
Baadhi ya wananchi na Wazee wa vijiji vya Jimbo la Uzini wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Umeme Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya wananchi na Wazee wa vijiji vya Jimbo la Uzini wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika hafla ya uzinduzi wa Umeme Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika asubuhi.
Akinamama waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Umeme Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika hafla ya uzinduzi wa Umeme.
Meneja wa Shirika la Umeme ZECO Hassan Ali Mbarouk alipokuwa akisoma Risala ya Shirika mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa Uzinduzi wa Umeme katika Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja. [Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment