Naibu Waziri wa Nishati na Madini
anayeshughulikia Madini, Mhe Stephen Masele (aliyesimama katikati na pama) akishuhudia
halfa fupi ya kusaini makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha
Madini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian
Chiragwile, katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje, na
kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Resolute Peter Beilby. Wengine wanaoshuhudia
ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi (wa pili kuchoto aliyesimama),Mkurugenzi
Kampuni ya Resolute Rose Aziz na baadhi ya waliohudhuria.
Meneja
Mazingira baada Mgodi wa Resolute
Jackie Sinclair (Kulia), akimkabidhi funguo mbalimbali za majengo ya eneo la
mgodi wa Resolute Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Stephen Masele (Kushoto) mara makabidhiano ya eneo la mgodi.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Chuo
cha Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe funguo mbalimbali za
majengo ya mgodi wa Resolute kwa ajili ya Chuo cha Madini Dodoma.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Resolute Perer
Beilby (wa pili kulia) akimwogongoza
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kukagua maeneo mbalimbali ya
Mgodi wa Resolute ambao yamekabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele akiangalia chumba cha Computer
ambacho ni miongoni mwa vifaa ambavyo Mgodi wa Resolute umekabidhi kwa ajili ya
Chuo cha Madini Dodoma.
Meneja Mazingira wa mgodi wa Resolute Jackie
Sinclair (mbelea) akieleza jambo wakati akikiabidhi baadhi ya vifaa vya maabara
kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Stephen Masele ujumbe alioambatana nao.
Meneja
Mazingira wa Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair akikabidhi moja ya vifaa ambavyo vitatumiwa na Chuo cha
Madini Dodoma kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo wakati wa halfa ya
kukabidhiana eneo la mgodi wa Resolute. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Stephen
Masele, Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje na Mkuu wa Wilaya ya
Nzega Bintuni Msangi
Sehemu mgodi ambao shughuli za uchimbaji zilikuwa
zikifanywa na mgodi wa Resolute ambao pia umekabidhiwa kwa Chuo cha Madini
Dodoma. Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe ameeleza kuwa,mgodi huo
utatoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu shughuli za uchumbaji.
No comments:
Post a Comment