Vibao vinavyoonyesha Mabasi yaendeko kutoka kwenye Kituo hicho.
Na Bashir Nkoromo, Kinondoni
Manispaa
ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imedhihirisha jitihada zake za
kwenda na wakati katika huduma zake, baada ya kuamua kutoa huduma ya
bure ya mtandao wa intrenet wa WiFi kwenye Kituo kipya cha Mabasi cha
Sinza, jijini Dar es Salaam.
Akizindua
huduma hiyo, jana, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda
alisema, mtandao wa WiFi umeunganishwa kwenye kituo hicho kupitia mkongo
wa mawasiliano kupitia Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Mwenda
alisema, mtandao huo utakuwepo usiku na mchana na kila mwenye kompyuta
au simu zenye uwezo wa kunasa Wi-Fi ataona katika simu au kompyuta yake
akitaarifiwa kuwepo mtandao wa bure wa KMC_FREE WiFi.
Alisema,
mdau atakachofanya ni kujinga bure na kuendelea kupata taarifa
mbalimbali zikiwemo za tovuti ya serikali na ya Manispaa hiyo ya
Kinondoni na nyingine zote atakazotaka.
Mwenda
alisema, baada ya kuweka mtandao kwenye Kituo hicho, mwakani Manispaa
hiyo itaweka mtandao huo wa WiFi kwenye Kata zote 34 za Manispaa hiyo.
Alisema,
mradi huo wa WiFi umegharimu sh. milioni 21, na Manispaa hiyo itakuwa
ikiendelea kulipia huduma hiyo sh. milioni 2 kila mwezi ambazo itakuwa
inalipa kwa mkupuo kwa mwaka.
Kuzinduliwa kwa huduma hiyo,
kumeifanya Manispaa ya Kinondoni kuwa ya kwanza nchini kote, na pengine
hata Afrika Mashiriki, kutoa huduma hiyo bure tena bila kutumia namba ya
siri.
Mwandishi wa habari hii
alishuhudia huduma ya aina hii kwa mara ya kwanza alipotembelea nchini
China, ambapo WiFi inapatikana bure kwenye simu hata ukiwa barabarani.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akibofya kompyuta kuzindua
huduma ya WiFi ya bure kwenye Kituo cha Mabasi cha Sinza, wilayani humo,
Ijumaa, Desemba 12, 2014
Mwenda akizungumza baada ya kuzindua huduma hiyo
Mwenda
akikata utepe kwenye chumba ilimo mitambo ya kuendesha mtandao huo wa
huduma ya WiFi kwenye Ofisi za Kituo hicho cha mabasi
Baadhi ya wafanyakazi katika ofisi hiyo yenye kugawa WiFi
Kweli:
"WiFi ya Manispaa ya Kinondoni inapatikana bure! vijana wakisema baada
ya kuipata WiFi iliyozinduliwa kwenye Kituo hicho cha Mabasi.
No comments:
Post a Comment