Waziri
katika Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Mheshimiwa Prof. Mark Mwandosya
alifanya ziara ya kutembelea Mamlaka za Udhibiti wa huduma za umma na
shughuli zingine za kiuchumi kwa nia ya kufahamu utendaji, mafanikio na
changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa na
Serikali kuyafanya. Ziara hiyo ambayo ilianza tarehe 21 hadi 23 Julai,
2014 ilihusisha Mamlaka za udhibiti za SUMATRA, EWURA, TCAA, TCRA, TIRA
na SSRA.
Katika
ziara yake hiyo Waziri Prof. Mwandosya alieleza kuwa madhumuni ya ziara
yake ilikuwa ni kujifunza na kubalishana uzoefu katika shughuli za
udhibiti hapa Tanzania. Waziri Prof. Mwandosya alieleza kuwa shughuli za
udhibiti Tanzania zilianza rasmi kwa kuanzisha Mamlaka za Udhibiti kwa
kujibu wa sheria zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania takriban miaka 10 iliyopita.
Waziri
Prof. Mwandosya alieleza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika
kutekeleza majukumu yao, Mamlaka za Udhibiti hapa nchini bado zina
changamoto nyingi ambazo inabidi kukabiliana nazo kwa kujifunza na
kubadilisha uzoefu. Kipindi cha miaka 10 kinatosha kuweza kutathimini
tulikotoka, tulipo na tunakoelekea. Hii ni pamoja na kuweka malengo ya
kukabiliana na changamoto za kuwa na uchumi mzuri kwa miaka kumi ijayo.
Waziri
Prof. Mwandosya aliendelea kueleza kuwa Mamlaka za Udhibiti zinapaswa
kujiuliza kuwa zimefanya nini katika kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa
na Serikali, nini kimesababisha wao kushindwa kutekeleza baadhi maeneo
yao ya udhibiti na kwa kiwango gani mahusiano yao na Serikali yamesaidia
au kuathiri utendaji wa mamlaka hizo. Na mwisho ili kupata suluhu
mamlaka zinashauri nini kifanyike ili mahusiano yao na Serikali yaweze
kuboresha utendaji wao.
Aidha
Waziri Prof. Mwandosya alitoa ujumbe kwa watendaji wa Mamlaka za
Udhibiti kuwa pamoja na kwamba vyombo vya udhibiti vilianzishwa kwa
ajili ya kusimamia huduma za umma (utilities) lakini kimsingi vyombo
hivyo vilianzishwa kwa lengo kuu la kuchangia katika maendeleo ya
kiuchumi katika nchi.
Waziri
Prof. Mwandosya alitoa angalizo kuwa kuna haja ya kuongeza wigo kutoka
kwenye udhibiti huduma za umma na kushirikisha pia udhibiti wa shughuli
za kiuchumi zikiwemo za bima na hifadhi ya jamii. Pamoja na mamlaka hizi
kusimamia sekta tofauti lakini zinakabiliwa na changamoto zinazofanana.
Kutokana na hali hiyo Waziri Prof. Mwandosya alishauri kuna haja kuwa na
chombo kimoja ambacho kitajumuisha vyombo vyote vya udhibiti kwa ajili
ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri
Prof. Mwandosya pia aliwaasa Mamlaka hizi za udhibiti kufanya kazi kwa
kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo badala ya kufuata
maelekezo au kufanya maamuzi ya kuwafurahisha wanasiasa. Muelekeo ni
kwamba kunakuwepo na huduma kwa umma ili wananchi waweze kuchangia
ipasavyo katika uchumi wa nchi.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti Nchi
Kavu na Majini (SUMATRA) alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo katika
ziara yake tarehe 21 Julai, 2014. Kushoto kwa Waziri Prof. Mwandosya ni
Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Bwana Gilliard Ngewe.
Baada
ya majadiliano na Uongozi wa SUMATRA Mheshimiwa Prof. Mark Mwandosya
alimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Bwana Gilliard Ngewe kitabu cha
Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Tanzania alichokiandika Prof. Mwandosya.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) alipotembelea ofisi za
Mamlaka hiyo katika ziara yake tarehe 21 Julai, 2014. Kulia kwa Waziri
Prof. Mwandosya ni Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA na kushoto kwake ni
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bwana Felix Ngamlagosi.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya pamoja na ujumbe wake wakifuatilia mawasilisho ya
taarifa ya utendaji ya EWURA iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa
EWURA Bwana Felix Ngamlagosi.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya akipata maelezo ya awali kutoka kwa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania Bwana James Diu alipowasili
katika ofisi za Mamlaka hiyo katika ziara yake tarehe 22 Julai, 2014.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya akiendesha majadiliano baada ya mawasilisho ya
taarifa ya utendaji wa TCAA yaliyofanywa na kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TCAA Bwana James Diu.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya na ujumbe wake akipata maelezo ya baadhi ya vifaa
vya kufuatilia mwenendo wa vyombo vya mawasiliano kutoka kwa wataalam wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRCA) mara alipowasili katika ofisi za
Mamlaka hiyo katika ziara yake tarehe 22 Julai, 2014.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya
Mawasiliano (TCRA) alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo katika ziara
yake tarehe 22 Julai, 2014. Kushoto kwa Waziri Prof. Mwandosya ni
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mamlaka
yaBima Tanzania (TIRA) alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo katika ziara
yake tarehe 23 Julai, 2014. Kushoto kwa Waziri Prof. Mwandosya ni
Kamishna wa Bima Bwana Israel Kamuzora na kulia kwake ni Naibu Kamishna
wa Bima Bwana Juma Makame.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya akipata maelezo ya awali kutoka kwa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii (SSRA), Dr. Carina Wangwe (Kulia) mara alipowasili katika ofisi
za Mamlaka hiyo katika ziara yake tarehe 23 Julai, 2014. Katikati ni
Meneja Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi Sarah Kibonnde.
Mheshimiwa
Prof. Mark Mwandosya akiendesha majadiliano baada ya mawasilisho ya
taarifa ya utendaji wa SSRA yaliyowashirikisha watendaji wa SSRA na
ujumbe wa Waziri Prof. Mwandosya.
No comments:
Post a Comment