Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani akifungua semina
ya siku mbili ya kimataifa inayozungumzia makabila ya asili, haki zao na
namna ya kuboresha maisha na mifumo ya chakula . Semina hiyo
inayofanyika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam inajiandaa kwa
kongamano la dunia nzima kuhusiana na jamii za asili ambalo litafanyika
Roma Italia, Februari 2015.
Mwakilishi Shirika la Kimataifa la maendeleo ya Kilimo, IFAD, Bw.Francisco Pichon akisisitiza jambo wakati wa kongamano hilo.
Washiriki
wa semina hiyo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakisikiliza kwa
makini mada mbalimbali zilizotolewa kuhusu haki za makabila ya asili na
namna ya kuboresha maisha yao na mifumo ya chakula .
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa kongamano hilo.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
No comments:
Post a Comment